Sheikh Ponda Issa Ponda (54) alipokelewa hapa Taasisi ya Tiba ya Mifupa
na Upasuaji wa mishipa ya fahamu (MOI) jana tarehe 11/8/2013 saa 7.30
adhuhuri akitokea Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Baada ya kupokelewa alionekana akiwa na majeraha chini ya bega la mkono
wa kulia lililokuwa limeshonwa mbele na nyuma madaktari wetu walifanya
uchunguzi na kushauri afanyiwe kipimo cha x-ray ili ubaini kama kuna
mvunjiko kwenye sehemu ya jeraha.
Tathimini ya madaktari baada ya kupata majibu ya x/ray ilionyesha
alikuwa na mvunjiko bila mifupa kupishana. Vivyo hivyo kidonda hakikuwa
katika hali nzuri licha ya tiba ya mwanzo na iliamuliwa afanyiwe
upasuaji mpya ili kuzuia maambukizi kama kingeachwa hivyo
KWA HIYO ….
Kufuatana na tiba ya awali aliyopata ikiwa ni pamoja na kushonwa jeraha
kabla ya kufikishwa MOI imekuwa vigumu kujua kama jeraha lilisababishwa
na kitu gani.
Kipimo cha x-ray kilionyesha kwamba alikuwa amepata mvunjiko wa mfupa mkubwa wa bega bila mifupa kupishana.
Hivyo basi sheikh Ponda Issa Ponda anaendelea na matibabu baada ya upasuaji.
Mkurugenzi Mtendaji,
Taasisi ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI)
No comments:
Post a Comment