Monday, August 5, 2013

TIMU ZA UFUNGUZI MPIRA WA PETE CHUO CHA MAENDELEO MBINGA MJINI, YAICHAPA BAMBO INVESTMENT

 Chuo cha maendeleo ya jamii(FDC) Mbinga mjini, ikiwa katika mashindano ya mpira wa pete ambapo aliichapa timu ya Bambo Investment ya mjini mabao 13- 9.  

Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.

LIGI ya Nanenane timu ya mpira wa pete wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, ambayo imeshirikisha timu tano imeanza kutimua vumbi hapa mjini jana kwenye uwanja wa michezo Mbinga mjini.

Zimetajwa timu hizo kuwa ni Bambo Investment ya mjini, Bambo Investment ya Myangayanga, Polisi, Chuo cha maendeleo ya jamii(FDC) Mbinga mjini, na Nyoni ambapo mashindano hayo yamedhaminiwa na Kampuni ya Bambo Investment yakisimamiwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mama Bambo.

Mashindano hayo yameratibiwa na ofisi ya Elimu, Michezo na Utamaduni wilayani hapa na maofisa utamaduni hao ambao ni Winfrida Amlani na Hussein Kanga kwa kushirikiana na Diwani wa viti maalum tarafa ya Mbinga mjini Grace Millinga ambapo kilele chake kitakuwa siku ya maadhimisho ya sherehe za Nanenane.


Akifungua mashindano hayo, mgeni rasmi Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga Idd Mponda alisema kuwa jambo la kuanzisha kwa mashindano limetoa hamasa kubwa kwa akina mama ili waweze kuonesha na kukuza vipaji vyao.

Mponda aliipongeza kampuni ya Bambo Investment kwa kuanzisha mashindano hayo na aliwataka wadau na wapenzi wa soka waweze kuiga mfano huo ili kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo vya akina mama wilayani Mbinga.

Timu za ufunguzi katika mashindano hayo zilikuwa Chuo cha maendeleo ya jamii(FDC) Mbinga mjini, ambapo aliichapa timu ya Bambo Investment ya mjini mabao 13- 9  na timu ya Polisi aliichapa timu ya Nyoni mabao 15 – 3.

No comments: