Na Steven Augustino,
Songea.
WAANDISHI wa habari mkoani Ruvuma, wameonywa kuamini habari kutoka mitandaoni na kuzitumia kuhabarisha umma bila kuzifanyia utafiti wa kutosha katika intaneti, na kutumia vyanzo vya kuaminika ikiwemo kuwahoji wahusika kupata habari za ukweli ambazo zitakuwa na manufaa kwa wasomaji.
Onyo hilo limetolewa na Simon Berege wakati wa mafunzo ya
kuwajengea uwezo wa namna ya kuandika habari kwa kutumia mitandao ya Intaneti
na kutuma picha za kihabari mtandaoni yanayoendeshwa katika Ukumbi wa
Veta, Manispaa ya Songea mjini hapa, na Taasisi ya Vyombo vya habari kusini mwa Africa (Media Institute
Of Southern Africa) MISA TANZANIA.
Wanahabari hao wamehitimu leo mafunzo hayo ambapo wamefundishwa
namna ya kufanya utafiti wa vyanzo vya habari mbalimbali katika Intaneti, na
kufungua njia nyingine za mawasiliano kama ‘youtube’, Blogu na namna ya
kuzitumia katika tasnia ya habari na kuzitengeneza zikiwa na takwimu sahihi.
Awali akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo ya
siku
tatu, afisa habari kutoka MISA -TANZANIA, Sengiyuva Gasirigwa, alisema
kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanahabari wa Ruvuma, ili
waweze kwenda na wakati hasa katika teknolojia ya kimtandao.
Wanahabari hao pia wananolewa ili waweze kujua kwa undani maana ya interneti, ‘World Wide Web’, ‘Computer’, na matumizi yake kwa manufaa ya maendeleo ya teknolojia, uchumi, siasa na utamaduni na kujali maadili ya kazi zao.
Gasiligwa alisema kuwa mafunzo hayo yanawahusisha Waandishi wa habari wa magazeti, televisheni na Rradio yanafanyika kwa ushirikiano wa MISATAN na shirika la VIKES toka Finland, na kwamba kwa kuanzia mafunzo hayo yalifanyika mkoani Pemba huko Zanzibar, na sasa mkoani Ruvuma na baadaye mkoa wa Mwanza.
Kadhalika naye mwezeshaji wa mafunzo hayo, Mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Tumaini Iringa, Saimon Berege, pamoja na mambo mengine
aliwataka wanahabari kuwa na ari ya kujiendeleza kielimu na kuwakaribisha
kwenda kusoma digrii ya pili (masters) inayotolewa na chuo hicho.
Kwa nyakati tofauti wanahabari hao nao waliipongeza taasisi hiyo kwa kuona umuhimu wa kutoa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari, huku
wakiongeza kwamba kuanzia sasa wataweza
kufanya kazi za uandishi wa habari wakiuchambuzi kwa kuoanisha habari kutoka vyanzo mbalimbali vya kimataifa, kuandika
habari kwa kutumia takwimu kutoka katika mitandao na kutumia taarifa na hotuba zilizopita zilizotolewa na viongozi wa kimataifa duniani.
Aidha washiriki hao wameonyesha ushirikiano mkubwa katika
uchambuzi wa
mada zilizotolewa na wameomba mafunzo kama hayo yaendelee kutolewa ili kuwajengea uwezo zaidi waandishi wa habari hapa nchini.
mada zilizotolewa na wameomba mafunzo kama hayo yaendelee kutolewa ili kuwajengea uwezo zaidi waandishi wa habari hapa nchini.
No comments:
Post a Comment