Monday, August 5, 2013

KILELE CHA MPIRA WA PETE LIGI YA NANENANE WILAYA YA MBINGA, KINATARAJIA KUFANYIKA SIKU YA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA NANENANE

Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Idd Mponda akitoa nasaha zake wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa pete ligi ya Nanenane Mbinga mjini, ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya Bambo Investment.

Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga, Idd Mponda ambaye ameshika mpira, akijiandaa kurusha mpira kuelekea miongoni kwa baadhi ya wachezaji, ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa mashindano ya ligi ya Nanenane mpira wa pete.

Mkurugenzi wa kampuni ya Bambo Investment(Mama Bambo) wa pili kutoka kushoto akijaribu kufanya mazoezi ya kukimbia mara baada ya mgeni rasmi kufanya ufunguzi wa mashindano hayo.

Kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Bambo Investment (Mama Bambo) akifuatilia kwa makini mashindano ya mpira wa pete amnbayo yalikuwa yakiendelea kufanyika katika uwanja wa mpira mjini hapa, katikati ni mgeni rasmi Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga Idd Mponda.

Mgeni rasmi Idd Mponda ambaye ni katibu tawala wa wilaya ya Mbinga, akimpongeza mwalimu wa michezo wa mpira pete.

Mgeni rasmi Idd Mponda aliyevaa nguo rangi ya njano, akiwakagua wachezaji wa mpira wa pete.

 

Wachezaji wa mpira wa pete wakiwa wanaimba wimbo wa Taifa, kabla ya mashindano ya mpira wa pete kuanza kwenye uwanja Mbinga mjini.

Wachezaji wakicheza mpira wa Pete, mara baada ya uzinduzi kufanyika ambapo mashindano hayo yatadumu kwa siku tano na kilele chake siku ya maadhimisho ya sherehe za Nanenane na mshindi atakayeshinda atakabidhiwa zawadi mbalimbali. (Picha zote na Kassian Nyandindi)

No comments: