Monday, August 5, 2013

UFUNGUZI WA LIGI YA NANENANE MBINGA YASHIRIKISHA TIMU TANO ZA MPIRA WA PETE, KAMPUNI YA BAMBO INVESTMENT YAPONGEZWA KWA KUDHAMINI MASHINDANO

Wachezaji wa mpira wa pete wakiwa wamejipanga mstari mmoja tayari kwa kuingia uwanjani kwa ajili ya ufunguzi wa mashindano ya ligi ya nanenane wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya BAMBO INVESTMENT. Aliyenyosha mkono ni diwani wa viti maalum tarafa ya Mbinga mjini, Grace Millinga akitoa maelekezo kwa wachezaji hao.

Vijana wakitoa burudani mchezo wa ngoma za asili eneo la uwanja wa mpira Mbinga mjini, kabla ya mashindano ya mpira wa pete kuanza.

Wachezaji wa mpira wa pete wakiingia uwanjani, kumpokea mgeni rasmi wa mashindano hayo.

Mgeni rasmi Idd Mponda ambaye ni Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, aliyevaa nguo rangi ya njano (Katikati) akiwasili katika uwanja wa michezo Mbinga mjini tayari kwa kufanya ufunguzi wa mashindano hayo, upande wa kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Bambo Investment ambaye hufahamika kwa jina maarufu Mama Bambo, akiwapungia mkono wachezaji na wananchi waliohudhuria katika mashindano hayo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Bambo Investment(Mama Bambo) akiwasalimia wachezaji na wananchi waliodhuria kwenye uwanja wa mpira Mbinga mjini.

Wachezaji wakiwa ndani ya uwanja wakibadilishana mawazo kabla ya mechi kuanza.(Picha zote na Kassian Nyandindi)


No comments: