Na Mwandishi wetu,
Tunduru.
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma
limechukua hatua ya kumshikilia dereva wa kampuni “Progressive Higleig Jv
Contractors”, inayojenga mradi wa barabara ambao kwa sasa unaosuasua wa kwa kiwango cha lami Kutoka wilaya ya Namtumbo hadi Tunduru, anayefahamika kwa jina la Philip Chigana kwa tuhuma za kusababisha mauaji.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo Deusdedith Nsemeki alisema hayo kwa waandishi wa habari na kuongeza kuwa katika tukio hilo pia
dereva huyo alimgonga mtoto wa miaka 12 na kumjeruhi vibaya.
Akifafanua taarifa hiyo alisema kuwa ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Mletele Manispaa ya Songea na kuongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi.
Alimtaja aliyefariki dunia kuwa ni mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Menas Mapunda na kusema kuwa majeruhi aliyelazwa katika Hospitali mkoa songea ni Emmanuel Komba.
Alisema dereva huyo aliyekuwa anaendeshag gari aina ya
Nissan duble cabin, yenye namba za usajili T. 857 BVR atafikishwa mahakamani wakati wowote
baada ya kukamilika kwa uchunguzi.
Akizungumzia hali ya majeruhi huyo mganga mafawidhi wa
hospitali ya mkoa wa Ruvuma, Dkt. Anton Ngaiza
alisema kuwa hali yake inaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment