Madini ya Urani yakionekana kujitokeza juu ya ardhi katika eneo la mto
Mkuju hifadhi ya Selous, wilayani Namtumbo.(Picha na Kassian Nyandindi) |
Namtumbo.
UVUMI
na kauli zilizokuwa zikielezwa na watu mbalimbali kwamba kazi ya uchimbaji wa
madini aina ya Urani katika mto Mkuju uliopo pori
la hifadhi ya Selous, wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma
kwamba umeanza sio kweli, badala yake kinachofanyika ni kukamilisha kazi ya
utafiti wa madini hayo.
Waandishi
wa habari wa wa mkoa huo wamefanya ziara maalumu ya kutembelea mradi wa mto huo
ambako kampuni ya Mantra Tanzania
inatarajia kuanza ujenzi wa mgodi wa madini hayo.
Kauli
zinazotolewa na watu mbalimbali ambapo wamekua wakidai mradi huo haufai kwa
kuwa unahatarisha maisha ya binadamu kutokana na athari za mionzi na uharibifu
wa mazingira.
Ilikuwa
ni ziara ya kikazi zaidi iliyowapa fursa waandishi wa habari wote wa Ruvuma
kuingia ndani ya Pori la hifadhi ya Selous, na
katika maeneo ambako utafiti umethibisha uwepo wa latili milioni 119 za madini
ya Urani, zitakazochimbwa kwa miaka 12 baada ya uwekezaji wa dola bilioni moja
za Marekani, utakaoiwezesha Tanzania
kuweka kibindoni mapato ya dola milioni 640.
Kwa
sehemu kubwa wanaharakati kutoka mashirika mbalimbali wamekuwa wakidai kwamba
mradi huo ni hatari kwa binadamu na mazingira.
Kilichopo sasa wataalamu wa kampuni ya Mantra Tanzania, wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi juu ya suala la utunzaji wa mazingira na athari za madini hayo, kabla ya kazi ya uchimbaji kuanza wakati wakisubiri kibali kutoka serikalini.
No comments:
Post a Comment