Na Steven Augustino,
Tunduru.
MKAZI mmoja wa kijiji cha Mbesa wilayani Tunduru,
mkoani Ruvuma ameuwawa kikatili, na wananchi
wenye hasira kali na mwili wake kuuteketeza kwa kuchomwa moto.
Aliyefanyiwa kitendo hicho cha kinyama ni Seif Jafari(18)
baada ya kumtuhumu ameiba simu.
Kabla ya mauaji hayo wananchi hao walimuangushia
kipigo kikali na kwamba
akiwa na wenzake wanadaiwa kuiba simu 6 ambazo zilikuwa zikichajiwa katika nyumba ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chikomo aliyefahamika kwa jina moja la Mwl. Komba.
akiwa na wenzake wanadaiwa kuiba simu 6 ambazo zilikuwa zikichajiwa katika nyumba ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chikomo aliyefahamika kwa jina moja la Mwl. Komba.
Walisema baada ya kufanikisha wizi huo marehemu na
wenzake waliondoka na kurejea Mbesa eneo ambalo alikutwa na wahanga watukio hilo wakati wakimtafuta.
Walisema baada ya kundi hilo la watu waliokuwa wakimtafuta kumkuta kijijini
hapo, marehemu alianza kuwakimbia baada ya kuwaona hali ambayo
iliwafanya wapige kelele za kuomba msaada kwa watu wengine.
iliwafanya wapige kelele za kuomba msaada kwa watu wengine.
Akizungumzia tukio hilo
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsemeki alisema polisi
wanaendelea kuchunguza chanzo cha tukio hilo.
Aidha Nsemeki alikemea tabia za wananchi hao kuchukua
sheria mkononi na kufanya mauaji, na kuwataka wasifanye hivyo badala yake watoe
taarifa katika vyombo vya ulinzi ili hatua
za kisheria ziweze kufuata mkondo wake.
No comments:
Post a Comment