Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu. |
Na Kassian Nyandindi, Uchambuzi.
NIMEKUWA
nikitafakari kwa kina juu ya tukio lililojitokeza siku kadhaa zilizopita katika
ziara ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, iliyofanyika
hapa wilayani Mbinga na Nyasa mkoani humo.
Tafakari
zangu zinaenda sambamba na mkuu wa mkoa huo Said Mwambungu kuwajia juu viongozi
wa wilaya hizo, baada ya kushindwa kumuandalia taarifa iliyo katika misingi ya
upembuzi yakinifu.
Binafsi
namuunga mkono Mwambungu, kwa kuligundua hili mapema na sitakosea nikisema hivi
sasa Taifa hili linahitaji viongozi walio makini kama
yeye na wenye kupembua mambo kwa haraka, ili tuweze kusonga mbele kimaendeleo.
Kitendo
cha uongozi husika, kushindwa kumuandalia kiongozi wa ngazi ya mkoa taarifa
inayochambua maendeleo ya wananchi katika sekta mbalimbali, inaashiria nini?
Na
je, hili linaleta maana gani kwa mtendaji wa serikali ambaye serikali
imekuamini na kukupatia ajira ukatumikie wananchi kwa kufuata misingi ya
utawala bora, na leo tunafikia mahali tunashindwa hata kutoa taarifa yakinifu
kwa kiongozi ambaye anakuja kukagua utekelezaji wa miradi hiyo ya wananchi?
Hizi
ni zama za ukweli na uwazi, tunaficha nini? yatupasa tuwe wazi katika kutoa
taarifa zetu na sio viongozi wanapohitaji taarifa za maendeleo ya wananchi
tunawapatia ambazo ‘hazijashiba nyama’
za kutosha, yatupasa tubadilike.
“Lawama hizi kwa kitendo kilichotokea Mbinga zimwendee
nani, kama sio watendaji husika waliopewa dhamana ya kuongoza wanakondoo wa
wilaya ya Mbinga, ambao siku zote wamekuwa wakituamini na leo tunawaangusha mbele
ya kiongozi wao wa mkoa wa Ruvuma, tuache uzembe tuwajibike ipasavyo”
Idara
ya mipango ndio inalojukumu kubwa la kujua maendeleo yote yanayofanywa katika sehemu
husika, lakini inashangaza kuona utekelezaji wa shughuli mbalimbali unashindwa
kuwasilishwa ipasavyo kwa viongozi wetu, hii ni aibu.!
Katika
kuyasemea haya ni vyema tubadilike na tufanye kazi zetu kwa misingi na taratibu
zilizowekwa, tuache kufanya kazi kwa mazoea, jamii ya wanambinga na taifa letu
kwa ujumla wanatutegemea sisi tulio madarakani katika mambo mbalimbali ya kusukuma
mbele maendeleo, hivyo yatupasa kuwa makini.
Mkuu
wa mkoa wa Ruvuma pongezi zikufikie endelea kuchapa kazi, kaza buti wanaruvuma
tupo mbele yako, Mungu ibariki Tanzania
na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Mwandishi
anapatikana kwa barua pepe nyandindi2006@yahoo.com
au 0762 - 578960.
No comments:
Post a Comment