Saturday, June 29, 2013

MWENYEKITI WA KUONGOZA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA APATIKANA LEO


Baadhi ya Madiwani wa CCM wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa chama hicho mjini hapa, mara baada ya kumaliza kazi ya kupiga kura ya kumchagua Mwenyekiti wao wa kuongoza halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.(Picha na Kassian Nyandindi)

Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.

WANACHAMA wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, leo wamekamilisha adhima yao ya kuwachagua viongozi watakao waongoza katika nafasi ya Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, uchaguzi ambao awali kulikuwa na mvutano na utata mkubwa ambao ulisababisha hata kuzua vurugu za hapa na pale.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida amani na utulivu vilitawala, huku askari polisi nao wakionekana kuwa imara katika viwanja hivyo vya ukumbi wa CCM mjini hapa, ambako uchaguzi ulikuwa ukifanyika.

Ni tukio la pekee ambalo wapenzi na wafuasi wa chama hicho leo hii, walikuwa wakilisubiri kwa hamu, juu ya nani ambaye anaweza kushika nafasi hiyo muhimu hapa wilayani.

Mara baada ya uchaguzi huo kufanyika Katibu wa Chama hicho Anastasia Amasi, alitangaza matokeo mnamo majira ya 8:35 ambapo alisema nafasi ya Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga imechukuliwa na ndugu Allanus Ngahi ambaye alipata ushindi wa kura 29.

MFALME MSWATI II AWASILI JIJINI DAR ES SALAAM

 

S
b2ap3_thumbnail_01.jpg 
Mfalme Mswati II kutoka nchini Swaziland, akishuka kwenye ndege yake wakati alipowasili jijini Dar es Salaam leo.


b2ap3_thumbnail_1_20130626-180459_1.jpg
Wasaidizi wake wakiimba nyimbo za kikabila kabla ya Mfalme wao kushuka ndegeni, haikuweza kufahamika kuwa ilikuwa ni mila za kwao au walikuwa wakitambika ama nini kilikuwa kikiendelea.


b2ap3_thumbnail_02.jpg
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Mfalme Mswati wa II wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo Mfalme Mswati wa ii, amewasili nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 'Smat Patnership' unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu.


b2ap3_thumbnail_04.jpg
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mfalme Mswati II, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,  leo.


b2ap3_thumbnail_03.jpg



b2ap3_thumbnail_05.jpg
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Mfalme Mswati II kutoka nchini Swaziland, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Juni 28, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 'Smat Patnership', unaotarajia kuanza Juni 28. Kushoto ni mke wa Mfalme Mswati.

Friday, June 28, 2013

UCHAGUZI WA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MBINGA KUFANYIKA KESHO

Christantus Mbunda, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbinga.



















Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.

UCHAGUZI wa nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma ambao uliahirishwa siku kadhaa zilizopita, sasa unatarajiwa kufanyika rasmi kesho Juni 29 Mwaka huu, katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliopo mjini hapa.

Kamati kuu ya chama hicho makao makuu ya taifa ilichukua jukumu la kuahirisha uchaguzi huo, kutokana na vuguvugu la kisiasa lililoshamiri mjini hapa ambalo linadaiwa kusababisha hata uchomaji moto wa ofisi ya Katibu wa CCM na kunusurika kuungua kabisa.

Vurugu hizo zinadaiwa kupinga ubabe uliokuwa umefanywa na kamati ya siasa ya mkoa huo,  ambayo inashutumiwa kukata jina la mgombea mmojawapo kimakosa kwa maslahi yao binafsi.

Ukataji wa jina hilo ambalo ni la Diwani Allanus Ngahi wa kata ya Kipapa, ulisababisha Wajumbe kugoma kufanya uchaguzi hadi watakapopata ukweli juu ya kwa nini jina hilo lilikatwa kimakosa au la.

UJUMBE WA OBAMA WAONYWA KUACHA LAPTOP HOTELINI NA KULA KACHUMBARI

Rais Obama.


Dar es Salaam, 
Tanzania. 
LICHA ya ujumbe wa Rais wa Marekani, Barrack Obama kutarajiwa kufikia katika hoteli kubwa zenye hadhi wakati kiongozi huyo atakapowasili nchini Julai Mosi mwaka huu, Ikulu ya Marekani imetoa tahadhari ya vyakula ambavyo hawatakiwi kuvigusa wakiwa nchini ikiwa ni pamoja na kutumia maji ya bomba.

Kwa mujibu wa taarifa ya maelekezo ya Ikulu ya Marekani, watu watakaokuwa kwenye msafara wa Obama wametakiwa kutotumia kachumbari. Pia imewataka kutumia maji ya chupa zaidi.

SHILINGI BILIONI 161 KUTUMIKA ULINZI WA SAFARI YA OBAMA AFRIKA

Rais Obama.
















Marekani. 

SAFARI ya siku nane ya Rais wa Marekani, Barack Obama katika nchi tatu za Afrika Senegal, Afrika Kusini na Tanzania  itaigharimu kati ya dola 60 na 100 ambazo ni sawa na kati ya Shilingi 161 bilioni na Shilingi 161 bilioni kwa ajili ya kuhakikisha Rais Barack Obama anapewa ulinzi wa hali ya juu.

Kiasi hicho cha fedha ni gharama za malazi,chakula pamoja na mambo mengine. Kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya uchumi wamesema fedha hizo zingilitosha kwa matumizi ya wizara tatu za Tanzania katika mwaka mmoja lakini kwa kuzingatia bajeti ya mwaka 2013/14 ambayo imetishwa juzi bungeni.

Kwa mujibu wa bajeti hiyo, Wizara au Ofisi ya Makamu wa Rais Shilingi 55.6 bilioni, Wizara ya Maliasili na Utalii Shilingi 75.6 bilioni na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Shilingi 30.3 bilioni.

WAANZA MAANDALIZI YA UJENZI WA KABURI LA MANDELLA

Mzee Nelson Mandella Madiba.

Pretoria,
Afrika Kusini. 

SERIKALI ya Afrika Kusini imeanza kuandaa mahali ambako rais wa zamani wa nchi hiyo atazikwa,  sambamba na ndugu kuelezwa kwamba wana haki ya kuondoa au kusimamisha mashine inayomsadia mzee huyo kuendelea kuishi.

Tayari gari linalotumika kuchimba makaburi limepelekwa kwenye eneo la makaburi ambako Mandela anatarajiwa kuzikwa. 

Lakini mbali ya hilo familia na maofisa wa serikali wamewasili nyumbani kwa Mzee Mandela, Qunu.

Kutokana na hali ya Mzee Mandela,  nchini Afrika Kusini hivi sasa kumekuwapo kwa shughuli nyingi nyumbani kwake, eneo la Qunu na pia katika Hospitali ya Pretoria ambako Madiba amelazwa kwa matibabu na makazi yake ya zamani-Mtaa wa Vilakazi, Soweto, pia mtaa kuko bize.

Monday, June 24, 2013

MANDELA MAHUTUTI HOSPITALINI
















Afrika Kusini. 

MADAKTARI wanaomtibu rais wa zamani wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela wamesema hali yake imekuwa sio nzuri kwa saa 24 zilizopita na sasa ni mahututi.

Habari hizo zimekuja kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais ya Afrika Kusini.

Taarifa hiyo imesema bado Mzee Mandela ameendelea kusalia hospitalini mjini Pretoria kwa siku ya kumi na sita akitibiwa mapafu yaliyosababisha tatizo kwenye mfumo wake wa upumuaji.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amemtembelea Mzee Mandela jumapili jioni na kuzungumza na jopo la matatibu wanaomtibia.

Baadaye bwana Zuma alirejea kauli yake ya kulitaka taifa na dunia kumuombea Mzee Mandela apate nafuu.(BBC Swahili News).

SOMA RATIBA YA OBAMA AKIWA TANZANIA


Dar es Salaam, 
Tanzania. 

IKULU ya Marekani na Idara ya Habari (Maelezo) Tanzania wametangaza rasmi ratiba ya Rais Barrack Obama atakapozuru Tanzania huku ikionyesha atakaa kwa siku mbili tu kuanzia Julai 1 na kuondoka Julai 2, mwaka huu.

Tanzania itakuwa nchi ya mwisho ya Afrika kutembelewa na Obama baada ya Senegal na Afrika Kusini. Atatua Senegal keshokutwa.

Mara atakapowasili Julai 1 na ndege yake kubwa ya Air Force One, Rais Obama atazindua barabara mpya katika upande wa mashariki wa geti la kuingia Ikulu.

Rais Obama, ambaye atafuatana mkewe Michelle pia siku hiyo ya Julai 1, pia atazungumza kwa nyakati tofauti na  kundi la wafanyabiashara kutoka nchi za Afrika na Marekani kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Friday, June 21, 2013

MAKAO MAKUU YA CCM TAIFA YASITISHA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA KUFUATIA VURUGU ZILIZOJITOKEZA

Madiwani wa Mbinga, wakitoka nje ya Ukumbi wa CCM wilaya ya Mbinga mara baada ya kupewa taarifa ya kusitishwa kufanyika kwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo.(Picha na Kassian Nyandindi)



Na Kassian Nyandindi,

Mbinga.

HALI ya kisiasa wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, imeendelea kuwa katika hali mbaya yaani sintofahamu, kufuatia Makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa kusitisha zoezi la uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, kutokana na vurugu zilizojitokeza.

Usitishaji huo umefanyika leo majira ya saa 10:00 baada ya Katibu wa CCM wa mkoa huo Verena Shumbusho kutoa taarifa mbele ya Madiwani wa wilaya hiyo kwamba, uchaguzi huo hauwezi kufanyika mpaka taarifa rasmi itakapotolewa kutoka ofisi ya makao makuu ya chama hicho.

Sababu za msingi za kutofanyika kwa uchaguzi huo zimebainishwa katika kikao hicho kilichoketi kati ya Katibu huyo, Madiwani na Uongozi wa Chama hicho wilaya ya Mbinga, ambapo Shumbusho alieleza bayana mbele ya Wajumbe (Madiwani) kwamba wawe na subira mpaka taarifa hiyo itakapotolewa juu ya kufanyika kwa uchaguzi huo, kwamba utafanyika lini.

BREAKING NEWS: OFISI YA KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYANI MBINGA YACHOMWA MOTO, YANUSURIKA KUTEKETEA






Hii ni ofisi ya Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, kwa nje mlango na madirisha nayo yalichomwa moto kama inavyoonesha katika picha.

Hili ni eneo la ndani ya ofisi ya Katibu wa chama cha Mapinduzi(CCM) wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, ambapo mapazia yaliyowekwa dirishani nayo yaliungua kwa moto.

Baadhi ya Madiwani wakiwa nje ya ukumbi wa CCM, wakitafakari juu ya tukio hilo la kuchomwa moto kwa ofisi ya Katibu wao.(Picha zote na Kassian Nyandindi)

Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida ofisi ya Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, imenusurika kuteketea kwa moto kufuatia watu wasiojulikana, kuichoma moto kwa kutumia mafuta aina ya petroli.

Ofisi hiyo imechomwa madirisha na mlango mmoja huku ndani yake mapazia yaliyowekwa madirishani, yakiwa yameteketea kwa moto.

Akizungumza na Waandishi wa habari Katibu wa CCM wa wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi alisema, tukio hilo la kuchomwa kwa ofisi yake limetokea usiku wa Juni 20 mwaka huu kuamkia leo.

Thursday, June 20, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU MLIPUKO WA BOMU ARUSHA HII HAPA

 


Inspekta Jenerali wa Polisi nchini, ametoa taarifa kwa vyombo vya habari, kisha amejibu maswali kadhaa, vitu vya msingi kwa sasa ni kuwa Taarifa Muhimu zitatolewa na Jeshi kwa wakati muafaka tena kwa usahihi, ila kwa leo amesema hadi sasa hakuna mtu anayeshikiliwa na jeshi kutokana na tuhuma za tukio hilo ingawa Ushirikiano umepatikana wa kutosha kutambua wajihi wa anayesadikiwa ndiye mtuhumiwa, lakini pili, Jeshi la Polisi litaifanyia kazi kauli ya Kiongozi mmoja wa Chama cha siasa aliyesema watu wasipochagua chama chao watakufa, watakufa kabisa.

Saturday, June 15, 2013

UCHAMBUZI: MGOGORO WA ELIMU MBINGA UTAENDELEA HADI LINI ?

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyoni kata ya Nyoni, Adolph Komba akifundisha wanafunzi wa darasa la saba wanaosoma katika shule hiyo wakati huu wa likizo ambao wapo katika kambi, alisema kuwa lengo la walimu hao kufundisha wakati huu wa likizo ni kuongeza kiwango cha ufaulu na maendeleo ya elimu ya msingi wilayani Mbinga.(Picha na Kassian Nyandindi)



 Na Kassian Nyandindi,

WAHENGA siku zote husema elimu ndio ufunguo wa maisha, na hakuna sehemu ambayo inaweza ikawa na maendeleo pasipo kuwa na elimu.

Katika hili hatuna budi viongozi tukawa na mipangilio mizuri ya kukuza sekta ya elimu katika maeneo yetu tunayofanyia kazi, kwa kujenga ushirikiano na kubuni njia mbadala za kukuza taaluma mashuleni.

Ni aibu kuona viongozi siku zote tumekuwa tukilumbana na kujenga migogoro ambayo inarudisha nyuma sekta hiyo muhimu, ambayo ndio msingi wa maendeleo katika jamii.

Katika makala haya napenda kuelezea mgogoro wa idara ya elimu shule za msingi, ambao umekuwa ukiendelea wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, na kusababisha baadhi ya vigogo kulumbana pasipo kuwa na sababu zozote za msingi.

Friday, June 14, 2013

MKUU WA WILAYA YA MBINGA AMSHUKIA KATIBU WA CWT, ASEMA NI KIKWAZO CHA MAENDELEO YA ELIMU WILAYANI HUMO

Upande wa kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbinga, Senyi Ngaga akizungumza na wadau mbalimbali wilayani Mbinga hivi karibuni.
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.

MKUU wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Senyi Ngaga amemshukia Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) tawi la Mbinga Samwel Mhaiki, akidai kwamba ni kikwazo cha maendeleo ya elimu wilayani humo, kutokana na katibu huyo kupenda kuendesha migogoro na kuchonganisha walimu mashuleni.

Ngaga alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake, juu ya maendeleo ya sekta ya elimu ya wilaya hiyo.

Alisema kuwa katibu huyo amekuwa kinara namba moja wa kupita mashuleni na kushinikiza walimu waache kufundisha (Wagome) hadi watakapolipwa madai yao, jambo ambalo alilieleza kuwa limekuwa likileta mgogoro usio na tija katika jamii.

WARATIBU WA ELIMU MBINGA NA MIKAKATI YA KUKUZA KIWANGO CHA ELIMU

Wanafunzi wakiwa katika kituo cha masomo (Kambi) katika shule ya msingi Mwanyu iliyopo kata ya Maguu wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma wakati huu wa likizo, ambapo Wadau mbalimbali wa elimu wamefurahishwa na mfumo huo ambapo wanasema mfumo huu kwa kiasi kikubwa utasaidia kukuza kiwango cha elimu wilayani humo.                                  (Picha na Kassian Nyandindi)


Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.

WARATIBU elimu kata wilaya ya Mbinga na Nyasa mkoani Ruvuma, kwa pamoja wameadhimia kuunganisha nguvu zao kwa pamoja ili kumaliza tatizo kubwa la kushuka kwa kiwango cha taaluma katika wilaya hizo, ikiwemo kuwafundisha kwa bidii watoto wanaotarajia kuanza mitihani ya kumaliza elimu ya msingi na sekondari, ili waweze kufanya vyema katika mitihani yao.

Aidha wamepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na afisa elimu ya msingi wa wilaya ya Mbinga Mathias Mkali,  ambaye amekuwa akijituma katika kuhakikisha kwamba walimu wanapata mahitaji yao ya    ya shule ikiwemo vifaa vya kutosha vya kufundishia.

Kufuatia jitihada hizo zinazoendelezwa na ofisa elimu huyo hivi sasa walimu na watoto mashuleni, wamekuwa wakijituma na kufanya vizuri  hali iliyoitoa wilaya hiyo kutoka nafasi ya tano hadi kufikia nafasi tatu  kimkoa, ikilinganishwa na matokeo ya miaka mitatu iliyopita kabla ya kufika kwake akitokea wilaya ya Tunduru ambapo wilaya hiyo ilikuwa ikishika mkia.

BAJETI CHUNGU: SIMU ZA MKONONI KUPIGWA USHURU




Simu ya mkononi.


















Dodoma, 
Tanzania.

WAMILIKI wa simu za mkononi nchini kuanzia mwezi ujao wataanza kuingia gharama kubwa ya kumiliki simu zao, baada ya serikali kuweka ushuru wa asilimia 14.5 ili kuongeza mapato ya Serikali na kugharamia elimu.

Kutokana uamuzi wa serikali sasa mmiliki wa simu atalazimika kutumia fedha nyingi kuigharamia ikiwa ni pamoja na kulipa fedha za kuchangia elimu achilia mbali kulipia muda wa hewani, na gharama nyingine ambazo mtu au watu wamekuwa wakikatwa na kampuni za simu kwa mfano nyimbo na ghama nyingine.

Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. William Mgimwa amesema hayo wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2013/14 unaonaza Julai Mosi mwaka huu.

Thursday, June 13, 2013

AFYA YA MZEE MANDELA YAENDELEA KUIMARIKA

 

 
Nelson Mandela.





















Hali ya Afya ya aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela, inaendelea kuimarika.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, aesema kuwa amefahamishwa na madaktari wanaomtibu kuwa, hali ya Mzee Mandela ambaye anaendelea kupokea matibabu katika hospitali moja mjini Pretoria imeimarika.

Rais Zuma amesema amefurahishwa na jinsi hali ya rais huyo inavyoendelea kuimarika, baada ya kudhohofika sana siku chache zilizopita.

CCM IKIPINGA SERIKALI TATU, CHIKAWE AJIPANGA KWA KATIBA YA BARA

 


    Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akifafanua jambo.
     

























    Editruda Mashimi, 
    Dar es Salaam.

    RASIMU ya Katiba mpya inayoruhusu muundo wa serikali tatu imezidi kukichanganya Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Chama hicho tawala kimepinga muundo huo kimesema bado kinaamini katika muundo wa Serikali mbili.

    Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwaambia kwamba mapendekezo yaliyofikishwa mbele ya tume hiyo yatabaki kama yalivyo,Na hivyo msimamo wao ni kuwepo kwa muungano wenye Serikali mbili kama ilivyo sasa.

    MAJI CHANZO CHA WANAWAKE KUBAKWA

     



















    Mwanamke akichota maji machafu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, kutokana na uhaba wa maji. (Picha kwa hisani ya Fullshangweblog)
















    Na Mwandishi wetu,

    WANAWAKE pamoja na watoto wa kike wa mkoa wa Shinyanga  Jimbo la Kishapu kata ya Mnhunze nchini Tanzania wanakabiliwa na matatizo ya kubakwa na kupigwa, kwa sababu ya shida ya maji.
    Mbali na matukio hayo pia wamekuwa wahanga wa kupigwa na waume zao baada ya kuchelewa kurudi jumbani kutokana na kwenda umbali mrefu kutafuta maji.

    Wakizungumza na mwandishi wetu, wanawake wa vijiji vya Mnhunze, Kisoso na Lubago wamesema kwamba mateso hayo pia wanakabiliwa na mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza kwa sababu ya kutumia maji yasiyostahili kwa matumizi ya binadamu ili kuepuakana na shida matatizo hayo hayo.

    Wednesday, June 12, 2013

    KATIBU WA CWT MBINGA AONJA JOTO YA JIWE, ANUSURIKA KUANGUSHIWA KIPIGO

    Katibu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilayani Mbinga Samwel Mhaiki akijibu tuhuma mbalimbali zinazomkabili ikiwemo matumizi mabaya ya ofisi na kuwachonganisha walimu na Serikali kwa kuandika barua zisizopata baraka kutoka kwa wanachama na kutowashirikisha viongozi wenzake ambapo alinusurika kipigo kutoka kwa walimu.


    Na Kassian Nyandindi,
    Mbinga.

    KATIBU wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma Samwel Mhaiki amenusurika kipigo kutoka kwa wanachama wa chama hicho, katika kikao na waratibu elimu kata wakimtuhumu kukitumia chama hicho kwa maslahi yake binafsi na kutotekeleza majukumu yake ipasavyo.

    Kadhalika wanachama hao walidai kwamba amekuwa akiwachonganisha walimu pamoja na viongozi wa serikali wilayani humo.

    Wakizungumza  huku wakiwa na  jazba na wengine kutoa lugha chafu kwa  Katibu huyo katika kikao kilichowakutanisha waratibu elimu kutoka kata zote za mbinga na nyasa, pia wamemtaka kuachia nafasi yake wakidai kuwa ameshindwa kuwasaidia katika kazi za utumishi wa umma.

    Tuesday, June 11, 2013

    KATIBU TAWALA MBINGA NA UZINDUZI WA MAGARI YA SUPERFEO EXPRESS

    Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga Idd Mponda akiwa amekaa ndani ya gari huku akiwa ameliwasha na kupiga honi....... ikiwa ni ishara ya kuzindua moja kati ya gari za kampuni ya Superfeo Express mjini Mbinga, ambazo zinataraji kuanza safari yake ya kutoka Mbinga kwenda Dar es Salaam mapema alfajiri kesho Juni 12 mwaka huu.( Picha na Kassian Nyandindi)

    KAMPUNI YA SUPERFEO EXPRESS, YAZINDUA MAGARI YAKE YA KUTOKA MBINGA HADI DAR ES SALAAM

    Magari ya Kampuni ya Superfeo Express, yakiwa pamoja katika eneo la Stand kuu Mbinga mjini yakisubiri kuzinduliwa tayari kwa safari ya kutoka Mbinga hadi Dar es Salaam.

    Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga, Idd Mponda akizundua magari ya Kampuni ya Superfeo Express katika eneo la Stand kuu Mbinga mjini, tayari kwa kuanza safari ya kutoka Mbinga mjini kwenda Dar es Salaam, gari hizo zinatarajia kuanza safari yake mapema alfajiri kesho, Juni 12 mwaka huu.

    Hapa Wadau wakifurahia mara baada ya uzinduzi huo kufanyika, ambapo kushoto ni Mwenuyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho, wa pili kutoka kushoto ni Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga Idd Mponda na watatu ni Mkurugenzi wa kampuni ya Superfeo Express Omary Msigwa.

    Hizi ni moja kati ya gari mpya mbili, za kampuni ya Supperfeo Express ambazo zitaanza safari yake kuanzia kesho alfajiri Juni 12 mwaka huu, kutoka Mbinga kwenda Dar es Salaam. (Picha zote na Kassian Nyandindi)

    CCM YAIPELEKA RASIMU KWA WANACHAMA WAKE





    Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana jana tarehe 10/06/2013 chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kikao hicho kilikuwa cha siku moja na maalum kwa ajili ya kupokea rasimu ya katiba mpya. 


    Kamati Kuu inaipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini kwa kazi nzuri na kukamilisha kazi kwa wakati.

    Kamati Kuu imepokea rasimu hiyo na kuelekeza kuwa;

    Kwa kuwa rasimu hii ni ya kwanza ambayo inapelekwa kujadiliwa tena kwa wananchi kupitia mabaraza mbalimbali ya katiba baada ya kuisha kwa hatua ya kutoa maoni.

    Kamati Kuu imekiagiza Chama kijipange kuijadili rasimu hiyo ndani ya Chama kama baraza la kitaasisi la katiba na kuwataka wanachama na wapenzi wa CCM wajitokeze kwa wingi na kushiriki kwenye mabaraza haya.

    Ushiriki huu wa CCM baada ya kupokea rasimu umekusudia kushirikisha wanachama wetu kwenye ngazi ya tawi, wilaya, mkoa na Taifa.

    Lakini pia Jumuiya za CCM zimekusudia kushiriki kama mabaraza ya Katiba na hivyo kuongeza ushiriki wa wanachama na wapenzi wa CCM katika mchakato huu.

    CCM kama baraza la katiba la kitaasisi litaipitia rasimu iliyowasilishwa kifungu kwa kifungu na kwa kuzingatia maoni ya CCM yaliyotolewa mwanzoni kabisa mwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba, wanachama wetu watashiriki kutoa maoni yao. 
     Pamoja na kazi nzuri ya Tume ya Mabadiliko ya katiba, Kamati Kuu inaiomba Tume hiyo kueleza vizuri mchakato mzima kutoka rasimu ya kwanza mpaka rasimu ya mwisho ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi juu ya mchakato mzima hasa baada ya rasimu ya kwanza kutoka.

    Kamati Kuu inawasihi Watanzania kushiriki tena kwenye kutoa maoni kupitia mabaraza ya katiba kwa rasimu ya kwanza, bunge maalum la katiba kwa rasimu ya pili na kupitia kura ya maoni kwa rasimu ya tatu, kwa amani,utulivu na kuvumiliana ili mwisho wa siku tupate Katiba nzuri ya nchi yetu kwa masilahi ya Watanzania walio wengi.
    Nape Moses Nnauye
    CCM Secretary for Ideology & Publicity.

    WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII BALOZI KHAMIS KAGASHEKI AFUNGUA MKUTANO WA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA TANAPA MKOANI IRINGA




    2aWahariri mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki wakati akifungua mkutano huo. 1a Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akifungua mkutano wa Shirika la Hifadhi za Mbuga za Taifa TANAPA na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu Wajibu wa vyombo vya habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za taifa unaofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo Ofisi za Manispaa ya Iringa, Balozi Kagasheki amewaasa wahariri wa vyombo vya habari kujadiliana kwa undani suala zima la kukomesha ujangili na jukumu la wanahabari katika mkakati huo wakishirikiana na serikali kwa ujumla kupitia taasisi za ulinzi katika mbuga za wanyama, amewataka wahariri kuwa wabunifu kwa kuandika makala na habari za kiuchunguzi ili kuibua mbinu hizo chafu na majangili ili kutokomeza ujangili huo na kupata ufumbuzi kamili wa changamoto hizo za ujangili, ameongeza kwamba wizara yake iko tayari kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wahariri na wadau mbalimbali yatakayofanikisha kupata ufumbuzi wa kutokomeza kabisa ujangili katika mbuga na pia amejiwekea utaratibu wa kukutana na waandishi wa habari kila mwezi atakutana na vyombo vya habari ili kuzungumza na wanahabari kuhusu masuala mbalimbali ya wizara hiyo.      3a 
    Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa makini katika kusikiliza wakati Waziri Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika mkutano huo.
    4a  
    5a 


     Balozi Khamis Kagasheki akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano huo kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo mjini Iringa
    Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma akizungumza katika mkutano huo wakati akimkaribisha Waziri wa Malisiali na Utalii Mh. Balozi Khamis Kagasheki.

    1  














    Waziri wa Malisili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma wakati akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Siasa na Kilimo mkoani Iringa ambako mkutano wa Wahariri wa vyombo vya habari na Shirika la Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA unafanyika. 
    3  

















    Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Ardhi Mazingira Ndugu James Lembeli akiingia kwenye ukumbi wa mkutano huku akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa TANAPA Ndugu Allan Kijazi kushoto.
      4 
    Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki wa pili kutoka kulia akiwa katika mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi na Mazingira Ndugu James Lembeli na kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa TANAPA Ndugu Allan Kijazi na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma.
      5 
    Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki katikati akiwa katika mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya Ardhi na Mazingira Ndugu James Lembeli na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma.
      6 
    Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akizungumza katika mkutano huo huku Waziri wa Maliasili Balozi Khamis Kagasheki wa pili kutoka kushoto akisikiliza, wengine ni Ndugu James Lembeli Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi na Mazingira na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma.
      7 
    Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya Ardhi na Mazingira Ndugu James Lembeli akizungumza katika mkutano huo huku waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akisikiliza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine 
    Ishengoma.(Picha na kikosi kazi cha Fullshangweblogspot.com)