Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Rachel Stephen Kassanda akihutubia
wananchi mbele ya Jengo la makaazi ya idara ya uhamiaji mkoa wa Ruvuma, mara baada ya kulizindua katika kata ya Mahenge Manispaa ya Songea. Amesema wapo wananchi wa mkoa wa Ruvuma wanaoshirikiana na Wahamiaji haramu
kuwasafirisha na kuwahifadhi katika maeneo maalumu amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa idara hiyo ili kutokomeza vitendo hivyo.
Kiongozi mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Rachel Stephen
Kassanda amesema wahamiaji walio wengi hutoka Eretria, Somalia hupitia mipaka
ya mkoa wa Ruvuma.
Pichani anayehutubia ni kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa 2014,
anayefuatia katikati ni Afisa uhamiaji mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza
na wa tatu kulia ni Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti.
Watumishi wa idara ya uhamiaji mkoa wa Ruvuma wakiwa katika picha ya
pamoja na Mwenge wa Uhuru katika jengo la makaazi la Afisa uhamiaji mjini Songea, lililozinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Rachel Stephen
Kassanda. Pichani aliye katikati ya viongozi wa mbio za Mwenge ni afisa uhamiaji wa mkoa huo Kokwi Lwebandiza.
Watumishi wa idara ya uhamiaji mkoa wa Ruvuma wakiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa mbio za Mwenge mara baada ya kuzindua jengo lao.
|
Mwenge wa Uhuru 2014 ukiwa na viongozi wa msafara wa mbio za Mwenge mkoani Ruvuma katika eneo la mradi
wa jengo la makaazi ya uhamiaji, Mahenge Manispaa ya Songea. Wenye sare
za kitenge ni kikundi cha kwaya kutoka wilaya ya Namtumbo. |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Zacharia Nachoa aliyeshika taarifa
akiwa katika msafara wa mbio za Mwenge Manispaa ya Songea kushiriki
katika uzinduzi wa miradi iliyokamilika katika halmashauri yake.
Katika utunzaji wa mazingira mkoa wa Ruvuma, kiongozi wa mbio za Mwenge
wa Uhuru Rachel Kassanda aliweza kupanda mti wa mkungu akiashiria kushiriki
katika utunzaji wa mazingira.
Afisa uhamiaji mkoa wa Ruvuma Kokwi Lwebandiza akipokea Mwenge wa Uhuru ikiwa ni ishara ya uzalendo nchini Tanzania.
Baadhji ya maafisa uhamiaji mkoa wa Ruvuma wakiwa na kiongozi wa mbio
za Mwenge wa Uhuru kitaifa Rachel Kassanda. kushoto ni Shaban, mmoja kati ya watumishi wa idara ya uhamiaji mkoani Ruvuma.
Hili ni jengo la uhamiaji mkoa wa Ruvuma lililozinduliwa na kiongozi wa mbio za
Mwenge wa Uhuru, kitaifa lililogharimu kiasi cha shilingi 434,100,170. Lililopo
Mahenge Manispaa ya Songea.
Pichani wa pili kutoka kulia afisa uhamiaji mkoa wa Ruvuma Kokwi
Lwebandiza, akiwa na watumishi wa idara hiyo muda mfupi kabla ya msafara wa mbio za Mwenge wa Uhuru, kuwasili katika eneo la jengo la uhamiaji tayari kwa
kuzindua.
Mhasibu idara ya uhamiaji mkoani Ruvuma, aliyeshika Mwenge katika eneo la jengo la makaazi ya uhamiaji mjini Songea. (Picha zote na Mwandishi wetu)