Na Steven Augustino,
Namtumbo.
KUNDI kubwa la Simba limeripotiwa kuvamia na kuanza kuua ng’ombe wa wafugaji katika vijiji vilivyopo kata ya Lusewa wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma, hali ambayo imewafanya wamiliki wa mifugo hiyo kuishi kwa wasi wasi.
Awali wanakijiji hao walikuwa wakidhani kwamba mifungo yao kuwa
ni wezi ndio wanaoiba, kutokana na kutojua ni nani anayehusika na upotevu wa
mifugo yao.
Hayo yamebainishwa na Mtendaji wakata ya Lusewa Abdallah Maniamba wakati alipokuwa akizungumza waandishi wa habari juu ya matukio hayo na
kuongeza kuwa, hali hiyo inatokana na ofisi yake kupokea taarifa kutoka
kwa mwananchi mmoja
aliyejitambulisha kwa jina la Habari Jamwana kuwa hivi sasa kuna
kundi kubwa la simba waliovamia katika maeneo yao na wanamaliza mifugo.
Maniamba alifafanua kuwa aliwaona simba watatu dume,
jike na mtoto wakinywa maji katika mto chimalilo wakati
akiwa anaoga maji.
Alisema kufuatia hali hiyo alilazimika kuacha
kuoga na kukimbia kwa kasi baada ya kuwaona simba hao wakinywa maji katika eneo hilo na kwenda nyumbani, hatimaye kutoa
taarifa kwa viongozi wa serikali ili wawajulishe wananchi wao juu ya maeneo yao kuvamiwa na wanyama hao.
Akizungumzia hali hiyo afisa mhifadhi wa wanyama pori tarafa ya Sasawala Hussein Sudi mbali na kukiri kuwa na taarifa hizo alisema kuwa upo ushahidi wa kutosha kuwa, katika eneo hilo kuna makundi ya simba ambao kwa sasa wameripotiwa kuwa wanamaliza mifugo.
No comments:
Post a Comment