Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Kikwete, akifungua kituo cha kisasa cha mabasi ya abiria Mbinga mjini mkoani Ruvuma. |
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Kikwete hatimaye amefanya
ufunguzi wa kituo cha kisasa cha mabasi ya abiria ambacho kimejengwa Mbinga
mjini mkoa wa Ruvuma, kwa thamani ya shilingi bilioni 2.1.
Fedha
za ujenzi wa mradi huo zimetokana na mkopo kutoka bodi ya mikopo ya serikali za
mitaa, ambapo majengo pacha ya ghorofa moja yamejengwa yakiwa na vyumba 112 vya
kufanyia biashara.
Aidha
majengo hayo yana sehemu ya kupumzika abiria, kuegesha magari, miundombinu ya
usafi, maji na ya tahadhari ya moto ambapo ujenzi wake umechukua muda wa miezi
39.
Awali
akitoa taarifa ya mradi huo mbele ya Rais Kikwete, Mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Hussein Ngaga alisema mradi huo umejengwa na
kampuni ya GNMS ya kutoka Iringa chini ya usimamizi wa wakala wa majengo hapa
nchini (TBA).
“Mheshimiwa
Rais lengo la ujenzi wa kituo hiki cha mabasi ni kutoa mazingira mazuri kwa
wasafiri wanaoingia na kutoka, kutoa ajira kwa wananchi kwa kuwawezesha kufanya
biashara sehemu yenye staha, kuongeza mapato ya ndani ya halmashauri yetu na
kuboresha mnadhari ya mji wa Mbinga”, alisema Ngaga.
Ngaga
alieleza kuwa halmashauri kwa shughuli zote zitakazo endeshwa katika eneo hilo
inatarajia kupata mapato ya shilingi milioni 324.6 kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment