|
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete. |
Na
Kassian Nyandindi,
Mbinga.
WASOMAJI
wetu wa mtandao huu mara ya mwisho tuliwaeleza kwamba tutaendelea kuwaletea
tuhuma zingine ambazo zinaonesha kuleta mashaka dhidi ya Afisa elimu msingi
Mathias Mkali wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, ambazo Mkurugenzi mtendaji wa
wilaya hiyo Hussein Ngaga anamtuhumu huku akijua fika kwamba anamuonea na
hazina ukweli wowote ambapo binafsi haziningii akilini kwa mtu mwenye akili
zake timamu, endelea kufuatilia sakata hili kupitia mtandao huu.............
Awali
tuliwafafanulia juu ya chanzo cha mgogoro huu kwamba kuhusiana na tuhuma
inayojieleza kwamba Afisa elimu huyo ameunda NGO yake inayofahamika kwa jina la
UWEKAMBI ambapo kirefu chake ni Umoja wa Waratibu Elimu Kata wilaya ya Mbinga.
Sasa nachukua safu hii kutaka kuelezea tuhuma zingine ambazo
Mkurugenzi huyo amemtuhumu Afisa elimu huyo na inanilazimu niziweke bayana juu ya ukweli wake.
Nikiachana
na tuhuma hiyo ya Umoja wa Waratibu Elimu Kata wilaya ya Mbinga, naingia
katika tuhuma ya Ununuzi na matumizi ya
mafuta ambapo Hussein Ngaga anamtuhumu Mkali kwamba ameiba mafuta na kuyatumia
yenye thamani ya shilingi milioni 25,547,500 yakiwemo Petroli lita 5,500 na
Diesel lita 5,500 yaliyoagizwa Mei 26 mwaka huu na mafuta ya nyongeza Petroli
lita 4,500 na Diesel lita 4,500 ikiwemo na vilainisho vyenye thamani ya
shilingi milioni 22,250,000 yaliyoagizwa Agosti 12 mwaka huu ambapo ukweli ni
kwamba;
Uchunguzi
uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kuwa mafuta haya yote
yaliombwa kwa Mkurugenzi huyo, ili kuwezesha uendeshaji wa mitihani 11 ya Mock
kata, Mock mkoa ambapo ulifanyika mtihani mmoja na shughuli za kujisomea watoto
wakati wa likizo yaani Makambi kwa darasa la saba.
Aidha
mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa darasa la saba, mtihani wa ufundi na
matumizi ya ofisi kama dharula za misiba na uhamisho kwa shule 227 na kata za
kielimu 38 ikiwemo pia na vituo vya makambi 42 mafuta hayo yalitumika katika
shughuli hizo.
Katika
mahitaji hayo ni mtihani pekee wa kumaliza elimu ya msingi ndio Mkurugenzi
Hussein Ngaga, alinunua mafuta Petroli lita 1,000 na Diesel lita 5,000 mnamo mwezi
Septemba mwaka huu, ambapo mafuta hayo yalitumika kusambaza mtihani wa kumaliza
elimu ya msingi na yalitumika ndani ya siku tatu na yakaisha.
Mahitaji
ya mafuta hayo hapo juu yaliombwa kwa kuzingatia kuwa toka mwezi Machi 2014, idara
ya elimu msingi wilayani Mbinga haikupewa mafuta ya uendeshaji mitihani ya mock
kata, wilaya na mock mkoa ambapo pamoja na idara kutopewa mafuta haikusimamisha
utekelezaji wa shughuli zake za kila siku yaani matokeo makubwa sasa (BRN).