Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete. |
Na
Kassian Nyandindi,
Mbinga.
WASOMAJI
wetu wa mtandao huu mara ya mwisho tuliwaeleza kwamba tutaendelea kuwaletea
tuhuma zingine ambazo zinaonesha kuleta mashaka dhidi ya Afisa elimu msingi
Mathias Mkali wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, ambazo Mkurugenzi mtendaji wa
wilaya hiyo Hussein Ngaga anamtuhumu huku akijua fika kwamba anamuonea na
hazina ukweli wowote ambapo binafsi haziningii akilini kwa mtu mwenye akili
zake timamu, endelea kufuatilia sakata hili kupitia mtandao huu.............
Awali
tuliwafafanulia juu ya chanzo cha mgogoro huu kwamba kuhusiana na tuhuma
inayojieleza kwamba Afisa elimu huyo ameunda NGO yake inayofahamika kwa jina la
UWEKAMBI ambapo kirefu chake ni Umoja wa Waratibu Elimu Kata wilaya ya Mbinga.
Sasa nachukua safu hii kutaka kuelezea tuhuma zingine ambazo Mkurugenzi huyo amemtuhumu Afisa elimu huyo na inanilazimu niziweke bayana juu ya ukweli wake.
Sasa nachukua safu hii kutaka kuelezea tuhuma zingine ambazo Mkurugenzi huyo amemtuhumu Afisa elimu huyo na inanilazimu niziweke bayana juu ya ukweli wake.
Nikiachana
na tuhuma hiyo ya Umoja wa Waratibu Elimu Kata wilaya ya Mbinga, naingia
katika tuhuma ya Ununuzi na matumizi ya
mafuta ambapo Hussein Ngaga anamtuhumu Mkali kwamba ameiba mafuta na kuyatumia
yenye thamani ya shilingi milioni 25,547,500 yakiwemo Petroli lita 5,500 na
Diesel lita 5,500 yaliyoagizwa Mei 26 mwaka huu na mafuta ya nyongeza Petroli
lita 4,500 na Diesel lita 4,500 ikiwemo na vilainisho vyenye thamani ya
shilingi milioni 22,250,000 yaliyoagizwa Agosti 12 mwaka huu ambapo ukweli ni
kwamba;
Uchunguzi
uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kuwa mafuta haya yote
yaliombwa kwa Mkurugenzi huyo, ili kuwezesha uendeshaji wa mitihani 11 ya Mock
kata, Mock mkoa ambapo ulifanyika mtihani mmoja na shughuli za kujisomea watoto
wakati wa likizo yaani Makambi kwa darasa la saba.
Aidha
mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa darasa la saba, mtihani wa ufundi na
matumizi ya ofisi kama dharula za misiba na uhamisho kwa shule 227 na kata za
kielimu 38 ikiwemo pia na vituo vya makambi 42 mafuta hayo yalitumika katika
shughuli hizo.
Katika
mahitaji hayo ni mtihani pekee wa kumaliza elimu ya msingi ndio Mkurugenzi
Hussein Ngaga, alinunua mafuta Petroli lita 1,000 na Diesel lita 5,000 mnamo mwezi
Septemba mwaka huu, ambapo mafuta hayo yalitumika kusambaza mtihani wa kumaliza
elimu ya msingi na yalitumika ndani ya siku tatu na yakaisha.
Mahitaji
ya mafuta hayo hapo juu yaliombwa kwa kuzingatia kuwa toka mwezi Machi 2014, idara
ya elimu msingi wilayani Mbinga haikupewa mafuta ya uendeshaji mitihani ya mock
kata, wilaya na mock mkoa ambapo pamoja na idara kutopewa mafuta haikusimamisha
utekelezaji wa shughuli zake za kila siku yaani matokeo makubwa sasa (BRN).
Aidha
kutokana na Mkurugenzi huyo kutotaka kuipatia idara hiyo mafuta kwa sababu
anazozijua yeye na matakwa yake binafsi, ililazimika kukopa na kununua mafuta
kwa fedha taslimu kuanzia mwezi Machi hadi Septemba mwaka huu hadi wakati Dokezo
la kwanza la lita 5,500 petroli na 5,500 diesel na Dokezo la pili la lita 4,500
petroli na lita 4,500 diesel yanaandikwa idara haikuwa na mafuta.
Hivyo
idara ya elimu ya msingi baada ya kuona shughuli zake inashindwa kuendesha
ipasavyo iliamua kufanya hivyo, huku ikitegemea kwamba mafuta iliyoomba endapo
ingeyapata kutoka kwa Mwajiri wake, ingeweza kulipia deni la mafuta
yaliyonunuliwa kwa fedha taslimu kwa kazi husika.
Wakati
mafuta hayo yananunuliwa kwa fedha taslimu idara ilitumia mtindo wa kuwasilisha
risiti na hati iliyosainiwa na Waratibu elimu kata ambao walipokea mafuta hayo
ikiwa ni kumbukumbu na kuiwasilisha kwa boharia ili mafuta yaliyoombwa kwa
madokezo yaliyotajwa hapo juu yakinunuliwa yatumike kama ushahidi kwa Mwajiri.
Uchunguzi
umebaini kuwa pamoja na ukweli kuwepo kwa kazi zinazoonekana ambazo zimefanyika
na idara ya elimu msingi wilayani Mbinga, lakini Mkurugenzi wa wilaya hiyo
Ngaga alikataa kuyalipa mafuta hayo huku akitumia kigezo cha makosa
yaliyofanywa na boharia wake kwa makusudi, ambapo badala ya kutunza kumbukumbu
alizopewa boharia huyo aliamua kutumia issue voucher, ledger na nyaraka zingine
za kiboharia kwa kuwasainisha madereva.
Katika
hili inadhihirisha kuwa kulikuwa na mpango uliosukwa kati ya boharia husika
(Jina tunalo) na Mkurugenzi huyo wa halmashauri hiyo, kwani cha kushangaza baada ya
tukio hilo Hussein Ngaga aliamua kuchukua jukumu la kumhamisha mtumishi huyo kwenda
idara nyingine wilayani hapa, na kuanza kutengeneza madai kwamba Afisa elimu
msingi Bw. Mkali alikusudia kuiba mafuta kwa nyaraka alizoziandika boharia
huyo, mpango ambao ulikuwa ukiimarishwa na Mkaguzi wa ndani wa halmashauri ya wilaya
hiyo Laston Kilembe.
Kwa
ujumla mafuta yote yaliyotajwa hapo juu, imebainika kuwa kwenye madokezo
hayakununuliwa kama ilivyodaiwa kwamba Afisa elimu msingi ameiba, na mpaka sasa
hayajaidhinishwa na kununuliwa na Mkurugenzi huyo na kwa ushahidi hakuna
Voucher wala Check iliyotoa mafuta hayo.
Badala
yake Mkurugenzi Hussein Ngaga yeye mwenyewe aliagiza lita 6,000 tu kwa ajili ya mitihani
ya kumaliza elimu ya msingi ambayo imefanyika hivi karibuni, na yalitumika kwa
siku tatu za mitihani iliyokuwa ikifanyika, ambapo idara haikubaki na mafuta
badala yake imebaki na madeni ambayo Mkurugenzi ameyakataa kuyalipa.
Utafiti
umeendelea kubaini kuwa katika kipindi cha mwezi Septemba mwaka 2014 idara elimu
ya msingi wilayani humo, haikupewa mafuta ilikuwa ikilazimika kununua mafuta
kwa fedha taslimu na kupata risiti toka kwa muuzaji ambapo mafuta
yaliyonunuliwa kwa ajili ya kutekeleza kazi mbalimbali za idara ni kama
ifuatavyo;
- Mitihani ya Mock mkoa na kata mitihani 12 zilitumika petrol lita 6,745.
- Masomo ya ziada yaani Makambi wakati wa likizo kwa vituo 42 zilitumika petroli lita 1,260 kwa ajili ya shughuli za kuendeshea umeme kwa njia ya Jenereta.
- Matumizi ya lita 2,103 za diesel yalitumika kwa ajili ya usafirishaji mitihani na matumizi ya ofisi katika idara.
Kwa
ujumla katika kufanikisha maendeleo yasiweze kudorola katika sekta ya elimu
msingi wilayani Mbinga, idara ililazimika kukopa fedha na huduma mbalimbali
kutoka kwa mchapaji wa mitihani, fedha za UMITASHUMTA na posho za Waratibu
elimu kata walizolipwa kupitia kusimamia mtihani wa kumaliza elimu ya msingi
2014 baada ya mwajiri kukataa kulipa fedha hizo kila mratibu alilazimika
kulipia deni la mafuta aliyoyatumia kwa mitihani ya mock mkoa na kata.
Imeelezwa
kuwa mafuta haya yote yalitarajiwa yalipwe kupitia madokezo yaliyozuiliwa na
huyo Mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo, baada ya kumtuhumu Afisa elimu msingi
kwa madai ya kuyanunua mafuta hewa jambo ambalo sio kweli.
Jambo
hili limekuwa likielezwa kuwa Waratibu elimu kata wakati wote wa utendaji wa
kazi za idara hiyo ya elimu ya msingi, katika shughuli za uendeshaji wa mitihani
wilayani humo, wamekuwa wakitumia fedha zao binafsi kutoka mifukoni mwao na
sehemu ya fedha za UMITASHUMTA hali ambayo wengi wao wanasema inawavunja moyo
na kukatisha tamaa ya kujitoa kufanya kazi.
Pamoja
na mambo mengine katika tuhuma hii ya mafuta, pia Mkurugenzi mtendaji wa wilaya
ya Mbinga Hussein Ngaga anamtuhumu Afisa elimu msingi wilaya hiyo Mathias Mkali,
kuwa ametoa mafuta kwa pikipiki za
Waratibu elimu kata kinyume na miongozo ya fedha.
Katika
tuhuma hii mtandao huu umebaini kuwa jambo hili sio kweli ambapo kikao cha kamati
ya mipango na fedha cha Desemba 20 mwaka 2013, ndicho kilichoridhia pikipiki binafsi
za waratibu elimu kata kupewa mafuta kwa kazi za serikali lengo kufanikisha
ukuaji wa taaluma wilayani humo.
Tumebaini
kuwa kwa tuhuma hiyo inaonesha wazi kuwa mwajiri yaani Mkurugenzi huyo, hana nia ya kuwawezesha
mafuta watendaji wake (Waratibu elimu kata) licha ya kujitolea pikipiki zao binafsi
kufanyia kazi za serikali.
Kwa
ujumla shughuli za uendeshaji wa mitihani ya mock kata zimeanza tangu mwezi
Januari 2013 hadi sasa, na kuna miaka miwili taratibu zilizokuwa zinatumika ni
hizi hizi na hakuna malalamiko yaliyojitokeza kutoka kwa wazazi, wananchi na
hata walimu wilayani humo kama anavyodai mkurugenzi huyo.
Badala
yake haijawahi kutokea kwa Mkurugenzi Hussein Ngaga kutoa ushauri wowote kwa
lengo la kurekebisha na kuboresha mfumo wa uendeshaji wa mitihani wilayani Mbinga, ambapo mfumo uliopo sasa umeonekana kuleta matunda mazuri ya ufaulu cha
kushangaza badala ya kusimamia misingi ya maendeleo katika sekta hiyo muhimu ya
elimu, muda mwingi amekuwa akielekeza tuhuma dhidi ya Afisa elimu msingi Bw.
Mkali na kufikia hatua ya kumsimamisha kazi jambo ambalo sasa limekuwa likizua
mgogoro mkubwa na kuwagawa viongozi wa ngazi mbalimbali wilayani humo kuwa
katika makundi mawili ambayo hayana tija kwa wananchi wa Mbinga.
No comments:
Post a Comment