Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda. |
Na
Kassian Nyandindi,
Mbinga.
TAARIFA
zilizotufikia hivi punde Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga
mkoani Ruvuma, Hussein Ngaga ameitisha kikao na Waratibu elimu kata wakiwemo
pia Watendaji wa kata wa wilaya hiyo kwa lengo la kujadili mikakati mbalimbali
ya maendeleo husika, ikiwemo suala la waratibu hao na watendaji kwa lengo la
kutaka kuwarubuni kwa namna moja au nyingine juu ya kukubalina naye katika
mgogoro ambao unaendelea sasa kati yake na Afisa elimu msingi wa wilaya hiyo
Mathias Mkali.
Kikao
hicho ambacho kinafanyika katika ukumbi wa Jumba la maendeleo mjini hapa, vyanzo
mbalimbali vya habari vimeeleza kuwa kukutana na watu hao kunatokana na
Mkurugenzi huyo kuendelea kupanga njama na kutangaza kwamba Afisa elimu huyo ni
mwizi, ili watendaji hao na waratibu wamkubali kwa kile anachokitaka yeye jambo ambalo wengi wao wamekuwa wakishangazwa nalo, huku wengine
wakieleza kuwa ni vyema Ngaga akaachana na mambo hayo badala yake awe mbunifu
wa mambo ya kimaendeleo na sio kuendekeza migogoro isiyokuwa na tija kwa jamii.
Walisema,
Mkurugenzi huyo tokea afike wilayani hapa ni mtu wa kuendekeza majungu na
migogoro isiyokuwa na msingi kwa wananchi wa Mbinga, huku wakihofia kwamba
endapo ataendeleza mambo hayo huenda wilaya hiyo ikarudi nyuma kimaendeleo.
Katika
hatua nyingine wengi wao walieleza kuwa tokea afike katika wilaya hii ni mwaka
mmoja sasa umepita, lakini amekuwa ni mtu wa kupenda migogoro na kupanga safu
katika idara mbalimbali kwa lengo la kutaka kuweka wakuu wa idara ambao yeye
anawataka kwa maslahi yake binafsi.
“Hivi
sasa badala ya kubuni mambo ya kimaendeleo yeye amekuwa ni mtu wa kutengeneza
migogoro tu na kupanga safu katika idara mbalimbali hapa wilayani, ni vyema awe
mtu wa kubuni maendeleo ili wananchi wa Mbinga waweze kunufaika na matunda
yake, tunachotambua serikali ilimleta hapa asimamie maendeleo sio kutengeneza
fitina na migogoro ambayo sasa inaturudisha nyuma”, walisema.
Pamoja
na mambo mengine walieleza kuwa wanashangazwa na hali hiyo ambayo Mkurugenzi
huyo anaiendeleza, huku wakiongeza kuwa huenda yeye binafsi akawa na matatizo
au upangaji huo wa safu ni mbinu za kutengeneza mianya ya kujinufaisha yeye
binafsi kwa namna moja au nyingine.
Kadhalika
habari zilizotufikia kutoka vyanzo mbalimbali vimeeleza kwamba Ngaga ni mtu wa
kupenda kugombana na kujenga migogoro isiyokuwa ya lazima kwa wafanyakazi wenzake, kama ilivyo sasa kwa hapa Mbinga, ambapo
akiwa kama Mweka hazina (DT) katika wilaya alizotoka akifanyia kazi alikuwa
hata hana maelewano mazuri na viongozi wenzake, kwa mfano Halmashauri ya wilaya ya
Kyela mkoani Mbeya na wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.
Wengine wanasema hata Mkurugenzi aliyekuwepo awali wilayani hapa na kuahamia wilaya ya Nyasa Shaibu Nnunduma, wakati anamkataa akihamiwa kuwa DT, alikuwa na maana yake hivyo sasa wanambinga wanajionea wenyewe kwa vurugu hizi anazozifanya ambazo hazina faida kwao.
Mwandishi
wa habari hizi, hivi karibuni alipomtafuta Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya
wilaya ya Mbinga Hussein Ngaga ofisini kwake alisema, “mimi nasema kama unataka
kwenda kuandika kaandike tu sina jambo la kusema katika hili”.
“Hata
waandishi wengine wenzako walikuja hapa, niliwaambia kama kuandika nendeni
mkaandike tu mimi siogopi”, alisema Ngaga.
No comments:
Post a Comment