Jumanne Sagini Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (OWM-
|
Na
Kassian Nyandindi,
Mbinga.
TUHUMA
nzito ambayo inaendelea kufukuta juu ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya
wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Hussein Ngaga, kudaiwa kutopeleka fedha
za Capitation kwa wakati mashuleni wilayani humo kadiri ya miongozo ya Mpango
wa Maendeleo Elimu ya Msingi (MMEM) unavyosema, umeibua mapya ambapo taarifa
zilizotufikia hivi punde Mkurugenzi huyo anahaha hapa na pale kwa kuwatumia
wahasibu wake wa halmashauri hiyo, kuhakikisha kwamba fedha hizo zinarejeshwa kwenye akaunti husika
haraka iwezekanavyo.
Vyanzo
vya uhakika kutoka katika halmashauri ya wilaya hiyo vimeeleza kuwa shilingi
milioni 54,725,000 ndizo anazodaiwa Ngaga kutozipeleka kwa wakati na hivi sasa
zimekaa zaidi ya mwaka bila kupelekwa mashuleni.
Walisema
licha ya wakaguzi wa mkoa huo kukagua katika kipindi kilichopita na kutoa hoja
hiyo Novemba 11 mwaka 2013, pamoja na
kikao cha kamati ya mipango na fedha kilichoketi Julai 10 mwaka huu kupitia
hoja hiyo hakuna utekelezaji uliofanyika hadi sasa.
“Hivi
ninavyo kuambia dokezo juu ya fedha hizi linakimbizwa kwa haraka sana ili
kuweza kuziba pengo hili ambalo linaleta doa kwake, na hatujui hizi pesa
kwa nini zimekaa muda mrefu bila kupelekwa kwa wahusika kwa muda
muafaka”, kilisema chanzo chetu ambacho kiliomba jina lake lisitajwe.
Katika
hatua nyingine Ngaga analalamikiwa na baadhi ya walimu wa shule za msingi
wilayani hapa kwamba hajawalipa fedha zao za kazi waliyoifanya ya kufundisha
muda wa ziada wakati walikizo.
Walifafanua
kuwa fedha wanazozidai ni za Desemba mwaka 2013 na kwamba baada ya idara husika
kuandaaa malipo na fedha hizo kutoka, aliamua kuzichukua yeye mwenyewe kwa
mtindo kwamba anaziazima lakini cha ajabu hadi leo hii walimu hao hawajalipwa.
Mwandishi
wa habari hizi alipomtafuta Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
Mbinga Hussein Ngaga, ili aweze kutolea ufafanuzi juu ya malalamiko hayo ambayo
hayaleti picha nzuri kwa mtendaji wa serikali ambaye umewekwa madarakani
kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, hakuweza kupatikana ofisini kwake.
Hata hivyo taarifa
za uhakika kutoka vyanzo mbalimbali zinasema kuwa kamati ya siasa ya wilaya hiyo leo Novemba 12 mwaka huu imechukua maamuzi ya kuketi na kujadili jambo hilo kufuatia Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Dokta Hussein Mwinyi alipokuwa wilayani hapa
Novemba 9 mwaka huu, kumuagiza Mkuu wa wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga kwamba
mgogoro huo unapaswa kumalizwa mapema na sio viongozi kuendelea kulumbana
badala ya kufikiria kufanya shughuli za maendeleo kwa manufaa ya wananchi na
kizazi kijacho.
Hata
hivyo Mwinyi alimuagiza Mkuu wa wilaya Ngaga, kuhakikisha Afisa elimu msingi
wilayani humo Bw. Mkali, anarejeshwa ofisini haraka iwezekanavyo huku tuhuma ambazo
anatuhumiwa akiendelea kuzijibu wakati akiwa ofisini.
No comments:
Post a Comment