Dodoma,
Tanzania.
Chama cha CUF na Chadema hivi punde Bungeni , vimekubali kuomba radhi
kutokana na vurugu zilizosababishwa na CUF yenye mrengo wa Kiliberali
na Chadema imemfanya hivyo kutokana na kuihusisha CUF na masuala ya
ushoga na usagaji.
Vyama hivyo vimeomba radhi baada ya Kamati ya Maadili ya Bunge
kufanya kikao kuanzia saa 11:00 jioni mpaka saa 2:30 usiku na
kukubaliana kila chama kumuomba spika radhi, na pia kuliomba Bunge radhi
kutokana na vurugu za jana.
CUF wamelazimika kumuomba spika radhi; kuomba radhi Bunge na kuwaomba
radhi Chadema kwa kumtukana Waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekeil Wenje wakati akisoma hutuba yake
ambayo ndani yake ilieleza sera za mrengo wa Kiliberali ambazo pamoja
na mambo mengine ni ushoga na usagaji.
Awali Mnadhimu wa Chama cha CUF Rashid, wakati akiomba radhi
aliipongeza Kamati ya Maadili na Chadema kwa kufikia muafaka kwa maslahi
ya Taifa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“ Napenda kuomba radhi kwa watu wote walioumizwa na vurugu za jana,” alisema Rashidi.
Naye Kiongozi wa Kambi rasni ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe
alisimama Bungeni na kuwaomba radhi CUF, Bunge na Spika
kutokana na hotuba ya jana iliyosomwa bungeni jana na Wenje.
Awali kabla ya kuomba radhi leo, Freeman Mbowe jana kwenye kikao cha
Kamati ya Maadili ya Bunge, alisema kwamba CUF wanafuata mrengo wa
Kiliberali ambao msingi wa sera zao ni shoga na usagaji na kwamba
hawakufanya kos.
Pia alisema CUF alimdhalilisha Wenje (Chadema), CUF
walichana hotuba yao na kuwaudhi na kuwakera Chadema.
Kutokana na hali hiyo CUF walishauriwa kuomba radhi jambo ambalo wametii amri hiyo leo asubuhi.
Wakati akisoma taarifa ya kamati hiyo John Chiligati ambaye ni
Mbunge wa jimbo la Manyoni mashariki alisema jana CUF walikiri kwenye
kamati hiyo kwamba wao ni wanachama wa mrengo wa Kiliberali, lakini
chama chao hakikubaliani na sera zote kama za ushoga na usagaji kwa kuwa
serikali imeshatoa msimamo kwamba haiungi mkono mambo hayo.
No comments:
Post a Comment