Dar es Salam,
Tanzania.
WAKATI Baraza
la Mitihani Taifa (NECTA) likitangaza matokeo mapya ya kidato cha nne, baada ya
kufanya marekebisho ya alama za viwango vya ufaulu, njama za kukwamisha
hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa
zinaandaliwa.
Habari zilizonaswa
kwa msaada wa vyanzo mbalimbali vinaeleza
kuwa, Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejipanga kukwamisha hotuba ya
Wizara hiyo, kwa madai kwamba Waziri huyo ameshindwa kusimamia sekta ya Elimu.
Vyanzo hivyo vinadai
kwamba, Wabunge wamepania kukwamisha hotuba hiyo na kumtaka Waziri huyo
ajiuzuru ili kukisafisha chama hicho kutokana na aibu ya mkanganyiko wa kufeli
kwa wanafunzi mwaka huu.
"Hotuba ya
Wizara ya Eilimu haiwezi kupitishwa kirahisi kama
Kawambwa hata jiuzuru, hatuwezi kuendelea kuwa na mawaziri wanaoshindwa
kuwajibika ipasavyo katika setka zao, kitendo cha mawaziri hao kushindwa
kuwajibika ipasavyo ndiyo kunachangia kuharibu Chama", kilisema chanzo
hicho.
"Huu mpango
unaendelea kusukwa na wabunge wa CCM waliopania kurudisha heshima ya chama, lazima
tuanzie ndani kuwajibishana wenyewe kabla ya wapinzani kuanza, kwani
tukishindwa sisi watatumia udhaifu wetu kuwashawishi wananchi, na hatimaye
watazidi kuichukia Serikali", kiliendelea kufafanua.
Wakati Waziri Kawambwa
akiandaliwa zengwe la kung'olewa, NECTA imetangaza matokeo yaliyoongeza kiwango
cha ufaulu kufikia asilimia kati ya 54 na 57 wiki hii, pamoja
na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
No comments:
Post a Comment