Monday, May 20, 2013

MAWAZIRI WATATU WA JAKAYA KIKWETE AMBAO WAKO HATI HATI KUTOLEWA, HAWA HAPA

  
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi  Dk Shukuru Kawambwa.

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk. Mathayo David Mathayo 
Dkt. Mathayo David Mathayo, Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi.

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhAGwjzsUVqfq3UijG9oxL4vlY6gQyP3eQAFOSljCMNGYldUBT_R_DGZMbDnj6bKKkXNpBr4bfFyDD2Wg8UZON6lNoAylCH47CvSyB9vkS7c7eGCQiH_kZxntuIx7IsQYoCPWrFvpjE9w4/s1600/Dk.+Fenella+Mukangara,+Waziri+wa+Habari,+Vijana,+Utamaduni+na+Michezo.JPG 
Dkt. Fenella Mukangara, Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.


Na Mwandishi wetu, 

UPEPO mbaya ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) unazidi kuvuma, safari hii wabunge wake wakimtaka Rais Jakaya Kikwete kuwafukuza kazi mawaziri watatu.

Mawaziri wanaotakiwa kung’olewa ni Dkt. Shukuru Kawambwa (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Dkt. Mathayo David Mathayo (Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi) na Dkt. Fenella Mukangara (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo).
Kama Rais Kikwete atakubali kuwaondoa madarakani mawaziri hao, hii itakuwa mara ya pili kwake kufanya hivyo. Mara ya kwanza ilikuwa Mei mwaka jana.


Mwaka jana Rais Kikwete aliamua kuwaengua madarakani baadhi ya mawaziri waliokuwa wakiandamwa kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo uwajibikaji mbovu.
  
Miongoni mwa walioenguliwa mwaka jana ni Dkt. Haji Mponda aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mustafa Mkulo (Waziri wa Fedha), William Ngeleja (Nishati na Madini na Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii).
 
Msimamo huo wa wabunge wameutoa jana katika kikao baina yao na Rais Kikwete kilichokuwa kikitathimini mwenendo wa Chama na utendaji wa Wabunge.


Chanzo chetu ndani ya kikao hicho kilieleza kuwa baada ya Rais Kikwete kutoa hotuba ya ufunguzi, baadhi ya wabunge walianza kuchangia, huku wengine wakishutumiana kwa kuvujisha siri za vikao nje kwa Waandishi wa habari.


Wabunge hao walidai kuwa mawaziri hao watatu wamekuwa mzigo kwa Serikali ya CCM, kutokana na utendaji wao kutokuwa wa kuridhisha.


Walisema matunda ya uwepo wa mawaziri hao kwenye wizara husika hayaonekeni, hivyo kumtaka Rais Kikwete awang’oe.


Waziri Kawambwa analaumiwa kwa kuzembea kwenye sekta ya elimu ambayo inazidi kushuka kiasi cha kuifanya serikali ifute matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana.


Walisema kufutwa kwa matokeo hayo ambayo asilimia 60 ya waliofanya mtihani walipata daraja sifuri, kunadhihirisha uwezo mdogo wa Dkt. Kawambwa.


Wakati Kawambwa akibanwa kwa hilo, wenzake Mathayo na Mukangara wanadaiwa kuwepo wizarani bila kuonesha ufanisi wowote.Wabunge hao walidai kuwa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi anayoiongoza Dkt. Mathayo ni nyeti na ilipaswa kuwa ya pili katika kuchangia pato la taifa baada ya Wizara ya Maliasili na Utalii.


Walimshambulia Dkt. Mathayo kuwa mzigo kwa wizara hiyo kwani alipokuwepo Dkt. Magufuli (Waziri wa Ujenzi) ilikuwa ikifanya vizuri tofauti na hivi sasa.

No comments: