Askofu Norbeth Mtega. |
Hizi ni sehemu ya nyaraka zinazothibitisha kujiuzuru kwa Askofu Norbeth Mtega. |
Kassian Nyandindi,
Songea.
ASKOFU mkuu wa jimbo kuu la Kanisa
katoliki Songea, Mhashamu Norbeth Mtega
amejiuzulu.
Taarifa za kujiuzulu kwa kiongozi huyo
zilipatikana jana majira ya mchana zikieleza kuwa Askofu Mtega, alikuwa
ametembelea Abasia ya Wabenediktini iliyopo Hanga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.
Mhashamu Mtega alipokuwa katika abasia
hiyo ya Hanga aliwatangazia waumini na watawa wa shirika la Wabenediktini kuwa,
kuanzia sasa yeye siyo Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Songea.
Alisema badala yake jimbo hilo litashikiliwa na Askofu wa jimbo la Iringa,
Taricisius Ngalalekumtwa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la maaskofu Tanzania mpaka
atakapopatikana kiongozi mwingine wa kushika wadhifa huo.
Kwa mjibu wa
kiongozi mmoja wa Parokia ya kanisa hilo ambaye
hakutaka jina lake
litajwe, alisema hizo ni
taarifa za kweli kuwa Mhashamu Askofu Mtega ametangaza kujiuzulu wadhifa huo.
Alisema hata wao
hawajui kilimkuta nini maana hata hajawahi kudokezwa kuhusiana na jambo hilo.
“Watumishi wote hatukujua
kinachoendelea tumeshangazwa kuwa Askofu Mtega anatamka kwa kinywa chake kuwa
yeye kuanzia sasa siyo Askofu mkuu wa jimbo hili la Songea, jambo ambalo wote
tulibaki midomo wazi na hatujui kuna nini,”alisema mtumishi huyo.
Baadhi ya waumini
wa kanisa Katoliki jimbo kuu la Songea katika maeneo mbalimbali mjini Songea,
nao walionyesha kushitushwa na taarifa hizo.
Askofu huyo
alilipokea jimbo hilo na kuliongoza baada ya
aliyekuwa Askofu wa jimbo hilo
marehemu Jacob Komba kufariki dunia.
No comments:
Post a Comment