Marehemu Albert Mangwea (kulia)enzi za
uhai wake, akiwa na M 2 The P ambaye yuko Hopitali bado, wasanii hao walikutwa
wakiwa hoi katika chumba kimoja nchini Afrika Kusini.
PRETORIA,
Afrika
Kusini.
WAKATI utaratibu
mzima wa mapokezi ya mwili wa marehemu Albert Mangwea, ukiendelea kufanyika
huko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam nyumbani kwa Baba mdogo wa marehemu, taarifa
kutoka Pretoria Afrika Kusini zinaeleza kuwa, mwili wa marehemu huyo utaanza
kufanyiwa uchunguzi wa kina leo kabla ya kusafirishwa kuja nchini Tanzania.
Jamira Saidi
anayeishi nchini Afrika Kusini alipozungumza kwa njia ya simu na Mwandishi wetu
alisema kwamba, mwili wa marehemu leo utaanza kufanyiwa uchunguzi wa kina na
jopo la Madaktari ili kujua sababu hasa ya kifo chake.
Jamira ambaye ni
kati ya Watanzania waliojitolea kuhakikisha kwamba ukweli wa kifo cha msanii
huyo unajulikana, tofauti na hivi sasa ambapo kila mtu anazungumza analo juwa.
Alisema wamekwisha
fanya mawasiliano na serikali ya Afrika Kusini kuhusu uchunguzi huo.
"Mimi pamoja
na baadhi ya Watanzania tunaoishi hapa Johanesburg na wengine waliopo Pretoria,
tumeamua kufuatilia na kusimamia ukweli wa jambo hili, leo uchunguzi wa
madaktari unaanza na tunatarajia kwamba utakamilika kesho na baada ya hapo
tutaanza utaratibu wa kusafirisha mwili wa marehemu, kuja nyumbani
Tanzania", alisema Jamira.
Akizungumzia hali
ilivyo Afrika Kusini hivi sasa Jamira alisema kwamba hali imetulia ingawa
watanzania wanaoishi katika maeneo mbalimbali nchini Afrika Kusini, wamepatwa
na mshutuko kufutia kifo cha Mangwea.
Kila mtu aliyepata
taarifa alijitahidi kuwasiliana na mwenzake na kupanga namna ya
kukutana. Kuhusu hali ya msanii M 2 The P aliyekuwa amepoteza fahamu hadi
jana jioni, Jamira alisema, hali yake kwa sasa ni nzuri madatkari wanaomtibu
jana walitoa taarifa kwamba ameweza kufumbua macho na kuzungumza ingawa
hawakusema alichokisema ila kwa ujumla hali yake imeanza kuwa nzuri.
|
No comments:
Post a Comment