Barack Obama. |
Dar es Salaam,
Tanzania.
Tanzania.
RAIS wa
Marekani, Barack Obama, atakuwa na ujumbe wa watu 700 katika ziara yake ya siku
mbili nchini Tanzania
kuanzia Julai Mosi mwaka huu.
Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe,
aliyasema hayo Dar es Salaam
jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema kutokana na ziara ya kiongozi huyo, alitoa wito kwa
wafanyabiashara wenye hoteli, migahawa, magari ya kukodisha waziboreshe
biashara zao ili Wizara hiyo iingie mkataba nao.
Aliongeza kuwa, akiwa nchini, Obama atafanya mkutano na viongozi
wa nchi zinazoendelea kwa kuzungumzia umuhimu wa sayansi na teknolojia katika
nchi zao.
“Ugeni huo ni mkubwa, ujio wa kiongozi huyu utaisaidia nchi kupata
pesa za Miradi ya
Changamoto za Milenia (MCC), ambazo zitatumika katika maji, elimu na barabara.
“Pia Rais Obama atazungumzia jinsi nchi za Afrika zitakavyopata
umeme wa kutosha tofauti na sasa...kimsingi tumejiandaa katika mapokezi yake
hata kwenye mavazi,” alisema Membe.
Hata hivyo Membe alisema tayari baadhi ya ujumbe ambao ataongozana
nao umeanza kuwasili nchini kwa matayarisho.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Haule,
alisema Umoja wa Nchi za Afrika (AU) sasa umefikisha miaka 50 tangu kuanzishwa
kwake.
Alisema maadhimisho hayo yatafanyika Makao Makuu ya umoja huo Addis Ababa, nchini Ethiopia
ambapo nchini Tanzania,
yatafanyika viwanja vya Karimjee, Dar
es Salaam.
Aliongeza kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo nchini atakuwa Membe
ambaye atakuwa na mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania.
Haule alisema umoja huo ulianza mwaka 1963 ambapo hadi sasa mafanikio
waliyoyapata ni ongezeko la wanachama
kutoka 32 hadi 54, kupatikana kwa uhuru wa nchi ya Sudan Kusini, viongozi wanawake barani Afrika na wananchi
kuwaheshimu viongozi wa nchi zao .
Alisema mbali ya mafanikio waliyopa ta pia kuna changamoto zilizopo
katika nchi wanachama kama tishio la ugaidi, uharamia na halitete katika
baadhiyanchi kama Somalia na
Mali. (Source Majira News paper)
No comments:
Post a Comment