MAELFU ya waombolezaji wamehudhuria katika mazishi ya
mtunzi mashuhuri wa vitabu barani Afrika, Chinua Achebe yaliyofanyika karibu na
nyumbani kwa familia yake mjini Ogidi, mji mdogo kwenye vilima vya jimbo la
Anambra.
Mwili wa marehemu Achebe
uliwasili nchini Nigeria
siku ya Jumatano, kutokea mjini Bostan, Marekani ambako alikuwa amefariki
dunia.
Mazishi hayo yalifanyika katika kanisa la
mtakatifu Philip la Anglikana, na kuhudhuriwa na waombolezaji ambao wamepewa
mualiko maalum huku wengine wakiwa nje wakisikiliza ibada hiyo, baada ya
kuwekewa spika.
Rais Goodluck Jonathan ni miongoni mwa waombolezaji
waliohudhuria mazishi ya mtunzi huyo mashuhuri wa vitabu barani Afrika, ambapo
katika mazishi hayo kulikuwa na ulinzi mkali katika mji mdogo wa Ogidi nchini
humo.
Mwandishi huyo mashuhuri alifariki mjini Boston, Marekani akiwa na
umri wa miaka 82 baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Hayati Achebe anasifika sana kwa kuwa mwanzilishi wa fasihi ya kiafrika
kwa luga ya kiingereza.
Kitabu chake alichokiandaa cha kwanza mwaka 1958,
Things Fall Apart, ambacho kilizungumzia sana
athari za ukoloni barani Afrika, aliweza kuuza zaidi ya vitabu milioni kumi.
Mwandishi huyo na msomi aliendelea na uandishi wake wa
kuandika vitabu vingine 20 baadhi vikikosoa wanasiasa, na kile alichokitaja
kama ukosefu wa uongozi nchini Nigeria.
Alikuwa anaishi nchini Marekani tangu mwaka 1990,
baada ya kupata ajali ya barabarani kumjeruhi kiasi cha kumpa ulemavu.
No comments:
Post a Comment