Dkt. Willbroad Slaa. |
Editruda Mashimi,
Dar es Salaam.
WAKATI Serikali
ikiendelea kuwatupia wanasiasa lawama kuhusiana na vurugu za wakazi wa Mtwara,
wanaopinga hatua ya Rais Kikwete na serikali yake kusafirisha gesi hadi jijini
Dar es Salaam kwa njia ya mabomba, Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willbroad Slaa, amesema
kwamba machafuko yanayotokea katika mkoa huo hayasababishwi na mambo ya
kisiasa, isipokuwa ni umaskini unaoikabili nchi.
Dkt. Slaa alisema
kwamba umaskini huo unaosababisha vurugu za Mtwara unachangiwa na CCM tangu
zama za kale na si kwa siasa za sasa.
“Yanayotokea
Mtwara ni matokeo ya umaskini ambao CCM imewaletea wananchi,
“Mtwara
wanakumbuka ya Mwadui, Geita na North Mara sasa wanayakataa”, alisema Dkt. Slaa
katika ukurasa wake wa Tweeter.
Alisema kwamba wananchi
hao wameamua kufanya yote hayo kwa kuangalia wenzao wa mikoa mingine
iliyojaliwa kuwa na mali nyingi katika mikoa yao, na bado hawanufaiki matokeo
yake inakuwa ni mali yakuwanufaisha wengine bila wao kupata faida yoyote ile.
Katika hatua
nyingine Dkt. Slaa alisema kwamba serikali isikimbilie kulaumu wanasiasa, bali
itambue kwamba siasa chafu zinafanya kazi kama watu ni maskini, lakini kama nchi itakuwa tajiri siasa chafu haziwezi kuwepo.
No comments:
Post a Comment