Askari wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Rodney Ndunguru, wakati wakielekea katika makaburi ya Mjimwema mjini Songea.
Mwili wa Rodney Ndunguru ukiingizwa katika kaburi.
Mama wa marehemu Rodney Ndunguru akiweka taji katika kaburi la mwanaye.
Na Mwandishi wetu,
Songea.
SIMANZI, vilio na majonzi vimetawala wakati wa mazishi ya askari wa Jeshi la
Wananchi Tanzania (JWTZ) Rodney Ndunguru wa kikosi cha makomando cha 92 KJ Ngerengere
mkoani Morogoro, ambapo mamia ya wakazi wa mkoa wa Ruvuma, wakiwemo askari
wa Jeshi la wananchi ambao walihudhuria mazishi hayo yaliyofanyika jana
kwenye makaburi ya Mjimwema Manispaa ya Songea.
Katika
mazishi hayo ambayo yaliongozwa na Paroko wa kanisa katoliki jimbo kuu
la Songea parokia ya Mjimwema padre Noel Duwe, ambaye wakati akiendesha
ibada ya mazishi aliwaonya Watanzania kutochezea amani na kwamba
utulivu walionao watanzania unahitajika kulindwa kwa namna ya aina
yeyote na sio vinginevyo.
Padre
Due alisema kuwa kwa wale wote wanaotaka kuchezea amani na utulivu
tulionao sasa, wanapaswa kukemewa kwa nguvu zote kwa kuwa watanzania
hatujazoea vurugu wala umwagaji wa damu jambo ambalo lilionekana kuvuta
hisia kwa watu waliofika kuomboleza msiba huo.
Aidha
Padri Due alimfagilia Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda
kwa kauli yake aliyoitoa Bungeni kuwa jeshi la Polisi lihakikishe linawadhibiti watu wanaoleta fujo kwa kupiga na kwamba kauli yenye
agizo hilo inapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote, badala ya kuibeza kwa
kuwa hivi sasa watu wengi wamekuwa wakidharau vyombo vya Dola wakidhani
kwamba serikali haipo.
Kwa
upande wake Kaimu wa Brigedi ya kanda ya Kusini Kanarli George Msongole
alieleza kuwa taarifa ya kifo cha Rodney, ilipokelewa muda mfupi baada
ya kifo chake na kuwa Jeshi la wananachi linaungana na familia ya
marehemu katika majonzi na msiba huo mzito.
Kwa
upande wake msemaji wa familia ya Marehemu Rodney Ndunguru alisema
kuwa familia imepata pengo kubwa kwa kuondokewa na kijana wao ,na
ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuisaidia ili waweze kujengewa
nyumba ambayo itwasaidia kwa kuishi mama yake mzazi na mjane.
Alisema
kuwa Rodney Ndunguru amefariki akiwa na miaka takribani miaka saba
kazini na akiwa na umri wa miaka 28 ambapo kimsingi kifo chake kimeacha
pengo kubwa katika famila kwani katika uhai wake ilikuwa farja kwa ndugu
na jamaa.
Rodney
Ndungu amezikwa saa 10:45 jioni kwenye makaburi ya Mjimwema ambako
mamia ya wakazi ya mkoa wa Ruvuma, walihudhulia akiwemo mwakilishi wa
mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ambaye ni Katibu tawala wilaya ya
songea Joseph Kapinga na kwamba mazishi yaliendeshwa kijeshi ambapo
askari wote walikuwa wamevaa sare huku wakifunga vitambaa vyeusi kwenye
mikono yao.
(habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment