Na Mwandishi wetu,
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dokta John Pombe Magufuli, ameridhia kuwapandisha vyeo maofisa 28 wa
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuanzia leo Aprili 12 mwaka huu.
Tukio hilo limeenda sambamba huku
akimbadilisha Msaidizi wake Kanali Mbaraka Mkeremy, ambaye amempandisha cheo na
atapangiwa kazi nyingine jeshini.
Kadhalika Rais Magufuli amekukubali
kumpandisha cheo kutoka Luteni Kanali kuwa kanali D.P.M Murunga na kuwa mpambe
wa Rais akichukua nafasi ya Kanali Mkeremy.
Vilevile akitoa taarifa ya uteuzi
huo, Mkuu wa Majeshi Jenelari Venancy Mabeyo alisema kuwa maofisa walioteuliwa
wanakwenda kuimarisha safu za utendaji kazi kijeshi na kwamba maofisa wote hao,
watavalishwa vyeo vyao Aprili 13 mwaka huu katika makao makuu ya Jeshi Upanga jijini
Dar es salaam.
Katika uteuzi huo amewapandisha vyeo pia
maofisa wa ngazi mbalimbali Jeshini ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya
Buhigwe Mkoani Kigoma, Kanali M E Gaguti ambaye sasa anapanda cheo na kuwa
Brigedia Jenelari na kurejeshwa jeshini.
No comments:
Post a Comment