Washiriki wa semina ambao ni watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali kutoka hapa wilayani Mbinga. |
Na Mwandishi
wetu,
Mbinga.
SERIKALI imeshauriwa kuendelea kuelimisha na kutoa mafunzo ya
kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI hususani kwa makundi maalum,
ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakitengwa katika jamii kwa namna moja au
nyingine.
Kutengwa huko imeelezwa kuwa ni kuwanyima fursa katika uelewa
wa mambo mbalimbali, jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya kizazi cha sasa na
kijacho.
Wito huo umetolewa leo kwenye semina ya siku moja, iliyolenga
kuwafanya watu wenye ulemavu kutambua haki zao za msingi na sheria ya watu
wenye ulemavu, ambayo imefanyika kwenye ukumbi wa Maktaba uliopo mjini hapa.
Semina hiyo imefadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la ‘The foundation for civil Society’
kutoka jijini Dar es Salaam.
Sambamba na hilo serikali imetakiwa kuendelea kutilia mkazo
na kufanyia utekelezaji mambo muhimu ikiwemo ujenzi rafiki wa miundombinu
mashuleni, ofisi na hata kwa taasisi binafsi nazo zimeshauriwa kuzingatia hilo.
Aidha vifaa ya kusomea ambavyo vinahitajika mashuleni kwa
kundi la watu wenye ulemavu, vinatakiwa viwepo ili kuliwezesha kundi hilo
liweze kusoma kwa urahisi.
“Katika shule zetu hakuna vifaa maalum vya kusomea watu wenye
ulemavu hususani kwa hawa wenzetu albino, viziwi na hata wasioona tunaiomba
serikali izingatie hili kwa kuhakikisha miundombinu rafiki kwa walemavu
inapatika mashuleni”, alisema Steven Matteso.
No comments:
Post a Comment