Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete. |
Na Kassian Nyandindi,
Ruvuma.
JESHI la polisi mkoani Ruvuma, linawahoji askari wake wawili
ambao wanadaiwa kuzembea wakiwa lindoni, na kusababisha watu wasiojulikana
ambao ni wezi kuvamia eneo la Ikulu ndogo wilayani Mbinga mkoani humo, na kufanya uhalifu.
Ikulu ndogo wilayani humo ndiyo ambayo anaishi Mkuu wa wilaya
hiyo Senyi Ngaga, huku baadhi ya wakazi wa mji wa Mbinga kufuatia tukio hilo
wamesema kwa nyakati tofauti kwamba, kuna kila sababu katika eneo hilo kutofanyiwa
mzaha na kuwepo na ulinzi wa kutosha kwa askari ambao waaminifu.
Uhalifu
uliofanywa na wezi hao ni kwamba walitoboa ukuta
wa chumba ambacho kuku hao walihifadhiwa, ambapo inadaiwa kuwa askari waliokuwa
lindoni hawakuwa makini katika kutimiza majukumu yao.
Wezi hao baada ya kuvamia katika eneo hilo Oktoba 2 mwaka huu
majira ya usiku, walifanikiwa kutoboa ukuta huo wa kibanda ambacho kimejengwa
kwa tofari, na kuiba kuku saba kati ya 28 ambao walikuwemo ndani yake.
Kamanda
wa polisi wa mkoa wa Ruvuma, Deusdedith Nsimeki amethibitisha kuhojiwa kwa
askari hao ambao majina yao hakuyataja, na kuongeza kuwa taarifa kamili juu ya
tukio hilo, itatolewa baadaye mara baada ya uchunguzi kukamilika.
No comments:
Post a Comment