Mji wa Songea. |
Na Muhidin Amri,
Songea.
WAKAZI wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, wametakiwa kutumia
maji kwa uangalifu kutokana na huduma hiyo kutolewa kwa mgao ambao
unasababishwa na ukosefu wa umeme wa uhakika katika Manispaa hiyo, kutokana
na mashine za kusukuma maji kwenda kwenye makazi ya watu kushindwa
kufanya kazi yake ipasavyo.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni, na afisa uhusiano wa Mamlaka
ya maji safi na mazingira (SOUWASA) Neema Chacha, alipokuwa akizungumza
na mwandishi wa habari hizi mjini Songea.
Chacha alisema kufuatia tatizo la umeme unaotolewa kwa mgao
mjini Songea, mamlaka hiyo hulazimika kutoa maji kwa mgao pele umeme
unapowaka na wao ndipo waweze kuwasha mashine zao.
Alisema kutumia jenereta pekee kufanya kazi za uendeshaji kuwa za gharama
kubwa, na Mammlaka kupata hasara.
“Wananchi ni vyema nao wafahamu kuwa mji wa Songea umeingia kwenye
tatizo kubwa la umeme, hivyo wanalazimika kutumia maji kwa uangalifu na
maji yanayototolewa sasa tunafahamu hayawezi kutosheleza watu wote ikilinghanishwa na kipindi cha nyuma”, alisema
Chacha.
Akizungumzia juu ya mgao huo ambao kwa sasa unaonekana kuwa kero
kubwa kwa wakazi wa Songea, Chacha alibainisha kuwa, mgao huo unatekelezwa kwa
maeneo yote ya mji huo, na hakuna eneo hata moja linalopendelewa hivyo ni
muhimu kwao kuzingatia ratiba za upatikanaji wa maji ili kuwaondolewa usumbufu
unaoweza kujitokeza.
Aidha ametoa wito kwa wananchi, hususani wanaoishi jirani na
vyanzo vya maji kama katika milima ya Matogoro, Luhira, na Chemchem kuepuka
tabia ya kuharibu vyanzo hivyo au kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kulima au
kuchungia mifugo katika maeneo hayo kwakufanya hivyo kunaweza kuleta madhara
makubwa ikiwemo kukauka kwa vyanzo hivyo.
No comments:
Post a Comment