MKuu wa mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu. |
Na Dustan Ndunguru,
Songea.
KITUO cha afya cha Mchoteka kilichopo katika wilaya ya Tunduru
mkoani Ruvuma kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa
watumishi, majengo na ukosefu wa dawa na vifaa tiba huku wagonjwa
wanaofika katika kituo hulazimika kutafuta huduma hiyo kwenye hospitali za
misheni kwa gharama kubwa.
Mganga mkuu wa kituo hicho Dokta Tigrida Sanga alisema kituo hicho
kinahudumia wananchi wa kutoka tarafa mbili ya Nalasi kwa
wilaya ya Tunduru na Sasawala, na kwa upande wa wilaya ya Namtumbo na nchi
jirani ya Msumbiji kutoka jimbo la Nampura.
Kituo hicho kinatoa huduma ya chanjo kwa wajawazito na
watoto, upimaji wa virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwa wajawazito na kutoa elimu ya
uzazi wa mpango, lakini wamekuwa wakikwama kutoa huduma hizo kutokana na
kukabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo pia upungufu wa watumishi, majengo na
vifaa tiba.
Alisema kwa sasa kituo kina watumishi wa sekta zote wapatao
saba kati ya 23 wanaohitajika, nyumba za watumishi zilizopo tatu kati ya 27,
hakuna jengo la maabara, hakuna jengo la upasuaji, jengo la ushauri
nasaha na hawana gari la kubeba wagonjwa, huku akidai hali hiyo inasababisha
watumishi wa kituo hicho
kufanyakazi katika mazingira mgumu.
Katika kuthamini mchango wa wananchi na serikali yao, wizara
kupitia halmashauri yao imeweza kutoa video kwa ajili ya kupeleka ujumbe kwa
wananchi juu ya kuwapatia elimu ya kujikinga na maambukizo ya magonjwa ya zinaa
na UKIMWI, lakini alidai video hivyo vimekosa mikanda na hivyo wananchi
wamekuwa wakiikosa elimu hiyo.
Alisema pamoja na kukabiliwa na changamoto nyingi za kiutendaji
bado kituo hicho kimekosa huduma ya nishati ya umeme wa jua (Solar)
kutokana na kuharibika na taarifa wameweza kutoa kwa idara husika, lakini
alidai hakuna kinachoendelea na kwamba kutokana na kukosekana kwa nishati hiyo
wagonjwa wanaolazwa kituoni hapo hulazimika kutumia taa za chemli kumulikia
wakati wa usiku.
No comments:
Post a Comment