Mji wa Songea. |
Na Muhidin Amri,
Songea.
WAKAZI wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, wametakiwa kutumia
maji kwa uangalifu kutokana na huduma hiyo kutolewa kwa mgao ambao
unasababishwa na ukosefu wa umeme wa uhakika katika Manispaa hiyo, kutokana
na mashine za kusukuma maji kwenda kwenye makazi ya watu kushindwa
kufanya kazi yake ipasavyo.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni, na afisa uhusiano wa Mamlaka
ya maji safi na mazingira (SOUWASA) Neema Chacha, alipokuwa akizungumza
na mwandishi wa habari hizi mjini Songea.
Chacha alisema kufuatia tatizo la umeme unaotolewa kwa mgao
mjini Songea, mamlaka hiyo hulazimika kutoa maji kwa mgao pele umeme
unapowaka na wao ndipo waweze kuwasha mashine zao.