Na Mwandishi
wetu,
Namtumbo.
WANANCHI wa
kijiji cha Mchomoro wilayani Namtumbo mkoa wa Ruvuma, wamepata msaada wa vifaa
vya ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho kutoka kwa Kampuni inayotarajia kuchimba
madini aina ya Uranium, Mantra Tanzania wilayani humo vyenye thamani ya
shilingi milioni 16,329,000.
Vifaa vya
ujenzi wa zahanati hiyo ilikabidhi ikiwa ni mchango wake katika kuungana na
wananchi wa kijiji hicho, kwa lengo la kukamilisha ujenzi wake ili uweze
kukamilika kwa wakati husika uliopangwa.
Ofisa habari
wa Kampuni hiyo, Khadija Pallangyo ndiye aliyekabidhi vifaa vya ujenzi kwa
uongozi wa kijiji cha Mchomoro ambapo alitoa msaada wa bati 425, saruji mifuko
400, nondo 51, misumari na waya kilo 40, boriti 10 na mbao 20.
Pallangyo kwa
upande wake aliutaka uongozi wa kijiji hicho kutumia vizuri vifaa hivyo kwa
lengo lililokusudiwa na sio kuingiza ubinafsi wa kutaka kujinufaisha watu
wachache.
Naye Kaimu
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Namtumbo, Laberto Mbilinyi pamoja na mambo
mengine aliutaka uongozi wa kijiji hicho kusimamia kwa umakini mkubwa juu ya
matumizi ya vifaa hivyo, ili kuwafanya hata wale wanaotoa misaada waweze kuwa
na moyo endelevu katika kusaidia wananchi.
Kwa ujumla
kijiji cha Mchomoro kimeomba kujenga kituo cha afya ambapo kwa hatua ya awali
kinatarajia kuanza na ujenzi wa zahanati kutokana na kijiji hicho kukosa huduma
za afya kwa wananchi wake kwa muda mrefu sasa.
Hata hivyo
Mchomoro kuna jumla ya kaya 897 na wakazi 8,531 ikiwa wanaume ni 4,122 na
wanawake 4,409 huku kikiwa na jumla ya vitongoji saba.
No comments:
Post a Comment