Na Kassian Nyandindi,
Songea.
SERIKALI kupitia Wakala wa Taifa Hifadhi ya Chakula (NFRA)
Kanda ya Songea mkoani Ruvuma, imelazimika kuongeza bei ya kununua mahindi ya
wakulima kufuatia kuwepo kwa ushindani mkubwa kutokana na wanunuzi binafsi
wengi wao mkoani humo, kununua mahindi kwa bei kubwa kutoka kwa wakulima
wanaozalisha zao hilo.
Aidha kufuatia kuwepo kwa ushindani huo, NFRA imeongeza bei ambapo
awali walikuwa wakinunua kwa shilingi 350 kwa kilo na kwamba kuanzia Novemba 7
mwaka huu wananunua mahindi kwa shilingi 580 kwa kilo maeneo ya vijijini na
shilingi 600 kwa wale wanaoleta katika kituo kikuu cha Ruhuwiko kilichopo mjini
hapa.
Kaimu Meneja wa Wakala huyo Kanda ya Songea, Majuto Chabruma alisema
hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya zoezi la ununuzi
wa mahindi linavyoendelea katika vituo mbalimbali vilivyotengwa katika wilaya
zote za mkoa wa Ruvuma.
Alisema kuwa katika msimu wa mwaka huu serikali ilitenga
shilingi bilioni 6.4 kwa ajili ya kununua mahindi tani 12,000 za awali mkoani
hapa, huku malengo yakiwa ni kununua tani 22,000 na kwamba bado
wanaendelea na kazi hiyo a ununuaji wa mahindi japo hawajafikia lengo husika
kutokana na kuwepo kwa ushindani mkubwa wa soko kutoka kwa watu na makampuni
binafsi.
Vilevile alibainisha kuwa serikali imeona ni vyema iongeze
bei ili kuweza kukabiliana na ushindani huo uliopo kwa lengo la kuweza kufikia
malengo iliyojiwekea ya kununua tani 22,000.
Alifafanua kuwa bado Wakala anaendelea na kazi ya kununua
mahindi ambayo bado yapo kwa wakulima na wauzaji wengine katika kituo cha
Ruhuwiko Songea na amewashauri wakulima mkoani Ruvuma, ambao bado wanayo ziada
ya mahindi majumbani kwao kwenda kuuza kwa Wakala huyo wa taifa wa hifadhi ya
chakula.
Kadhalika aliongeza kuwa hatua hiyo itaiwezesha
serikali kufikia malengo yake na nchi kwa jumla, ili iweze kuwa na akiba ya
chakula cha kutosha na kuwezesha kutoa nafaka hiyo pale patakapojitokeza uhaba
wa chakula mahali popote hapa nchini.
Pia Chabruma amewataka wakulima kuwa na kumbukumbu ya kutunza
akiba ya chakula na kuacha kuuza yote kwa wafanyabiashara kwani wasipozingatia
hilo wataweza kukaribisha njaa majumbani kwao.
Hata hivyo amewakumbusha wakulima mkoani Ruvuma, kuanza
maandalizi ya msimu mpya wa kilimo cha zao la mahindi kufuatia mvua tayari
zimekwisha anza kunyesha katika baadhi ya maeneo mkoani humo, badala ya
kusubiri katikati ya msimu jambo ambalo linaweza kusababisha wakulima kupata
mavuno kidogo kutokana na kuchelewa kwa maandalizi ya uzalishaji.
“Sisi kama halmashauri tayari kuna maeneo tumeyatenga kwa
ajili ya shughuli za kilimo, idara ya ardhi ipo tayari kutoa kila aina ya
ushirikiano kulingana na mwekezaji husika atahitaji kuzalisha zao gani”,
alisema.
Pia Hyera alibainisha kuwa mbali na kutenga maeneo
kwa ajili ya shughuli hizo vilevile wanaendelea kuuza maeneo mengine kwa
ajili ya viwanja vya ujenzi wa nyumba za makazi na biashara, ambapo viwanja
zaidi ya 742.
No comments:
Post a Comment