Friday, May 5, 2017

MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU MADABA MKOANI RUVUMA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge upande wa kushoto, akipokea Mwenge wa Uhuru jana kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka katika kijiji cha Mahanje halmashauri ya wilaya ya Madaba mara baada ya Mwenge huo kumaliza mbio zake mkoani Njombe tayari kwa kuanza mkoa wa Ruvuma.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Amour Hamad Amour, akimsikiliza Mwenyekiti wa Mahanje SACCOS wilayani Songea, Arika Mgina mara baada ya kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Saccos hiyo na kupongeza uongozi kwa kazi nzuri inayofanya ya kuwainua wananchi kiuchumi wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Madaba Shafi Mpenda na wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Songea, Pololet Mgema.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017, Amour Hamad Amour akiinua ndoo ya maji jana mara baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji safi na salama katika kijiji cha Lilondo halmashauri ya wilaya ya Madaba, wakati wa siku ya kwanza ya mbio hizo za Mwenge wa Uhuru mkoani Ruvuma, kulia ni mkazi wa kijiji hicho Ostella Mwenda.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Amour Hamad Amour na mkimbiza Mwenge kitaifa, Frederick Ndahani wakiomba dua ya kuwaombea waasisi wa Mwenge wa Uhuru Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume katika kijiji cha Lutukira halmashauri ya wilaya ya Madaba, mara baada ya kukagua kikundi cha vijana waendesha boda boda wanaojishughulisha na kilimo cha mahindi kijijini hapo, katikati ni mkazi wa kijiji hicho ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari St. Getruda katika halmashauri ya wilaya ya Madaba wilayani Songea mkoa wa Ruvuma wakiulaki Mwenge wa Uhuru jana ambao ulifika shuleni hapo kwa ajili ya kutoa ujumbe wa Mwenge kwa mwaka 2017 ambapo kiongozi wa Mwenge kitaifa Amour Hamad Amour aliwataka wanafunzi hao kuhakikisha wanaongeza bidii katika masomo yao ili waweze kufanikisha ndoto walizonazo kimaisha.


No comments: