Wednesday, May 24, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA KAMATI MAALUM ILIYOFANYA UCHUNGUZI WA MCHANGA WA MADINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, akipokea taarifa ya uchunguzi wa mchanga wa madini mbalimbali uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini hapa nchini, kutoka kwa Mwenyekiti wa kamati hiyo Profesa Abdulkarim Hamis Mruma leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Dkt. John Magufuli Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, akiangalia taarifa hiyo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali ya madini hapa nchini, mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Ikulu Jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wa kwanza upande wa kulia wakishuhudia tukio hilo.
Dkt. John Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea ripoti hiyo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi, kutoka kwenye machimbo mbalimbali ya madini hapa nchini.
Nao viongozi mbalimbali wa dini na siasa hawakuwa mbali na tukio hilo wakifuatilia taarifa ya ripoti hiyo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Injinia John Kijazi, Mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi wa mchanga wenye madini Profesa Abdulkarim Hamis Mruma pamoja na Wajumbe wa kamati hiyo mara baada ya kuipokea leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Ikulu)


No comments: