Katibu wa Mbunge Jimbo la Mbinga mjini, Geddy Ndimbo aliyevaa kofia akimkabidhi baiskeli maalumu (Wheel chair) mlemavu, Franko Tinda ambaye amekaa kwenye kiti. (Picha zote na Kassian Nyandindi) |
Na
Kassian Nyandindi,
Mbinga.
MBUNGE
wa Jimbo la Mbinga mjini mkoani Ruvuma, Sixtus Mapunda ametoa msaada wa
baiskeli maalumu (Wheel chair) ya kutembelea mlemavu Franko Tinda (21) ambaye
ni mkazi wa kata ya Kitanda wilayani humo yenye thamani ya shilingi 500,000.
Akikabidhi
msaada huo mbele ya uongozi wa kata hiyo, Katibu wa Mbunge huyo Geddy Ndimbo alisema
kuwa baiskeli hiyo ya kutembelea mtoto huyo imepatikana kutokana na jitihada
zilizofanywa na Mbunge Mapunda.
Ndimbo
alisema kuwa jitihada hizo zilifanywa kwa lengo la kumsaidia Franko aweze
kuondokana na taabu alizokuwa akizipata kwa kutambaa kwa mikono na magoti,
hivyo aliona kuna kila sababu ya kumtafutia chombo hicho ili kuweza kumrahisishia
asiendelee kupata adha hiyo.
“Nakukabidhi
baiskeli hii iweze kukusaidia na kukurahisishia uweze kutembea vizuri, nawaomba
muendelee kumtunza vizuri mtoto huyu kama walivyo wenzake ambao hawana matatizo
ya ulemavu tunapaswa kumjali na kumpatia ushirikiano wa kutosha pale
anapohitaji msaada kutoka kwetu,
“Naomba
pia hii baiskeli itunzwe vizuri itumike kwa matumizi yaliyokusudiwa kwani nina
hakika sasa kitendo cha kumpatia hiki chombo tumeweza kumpunguzia adha
alizokuwa anazipata hapo awali”, alisema Ndimbo.
Vilevile
naye Kaimu Afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya mji wa Mbinga, Alphonce
Njawa alitoa rai kwa wananchi wa kata hiyo kwamba ni muhimu sasa wayatambue
makundi maalumu kwa kuwajali na sio kuwatenga au kubagua kwa namna moja au
nyingine.
Njawa
alikemea tabia ya wazazi wasiwe wanawafanyia vitendo vya ukatili watu wenye
ulemavu kama vile kuwafungia ndani kwani kufanya hivyo ni kuwanyima fursa
muhimu ambazo wanapaswa kuzipata.
“Tusiwe
tunawatenga hawa wenzetu kwa kuwafungia ndani, wazazi tukifanya hivi tutakuwa
tunakosea hivyo tuwajali kwa kuwapatia haki sawa kama walivyokuwa watu wengine
ambao hawana ulemavu tuache kuwanyanyapaa”, alisisitiza Njawa.
Pia kwa
upande wake akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo mzazi wa mtoto huyo
mlemavu, Michael Tinda alisema kuwa anamshukuru Mbunge huyo kwa kumpatia baiskeli
hiyo ambapo alisema ni mkombozi mkubwa kwake kwani awali alikuwa akipata shida
namna ya kutembea hasa nyakati za masika pale mvua zinaponyesha.
Alieleza
kuwa wakati huo wa mvua walikuwa wakilazimika muda mwingi kumbeba mtoto huyo hivyo
baada ya kupata baiskeli hiyo sasa ataweza kutembea vizuri bila kupata usumbufu
wa aina yoyote ile.
Kadhalika
Diwani wa kata hiyo, Zeno Mbunda akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake
waliokuwa wamewasili wakati wa kupokea kiti hicho cha kutembelea mlemavu huyo alitoa
shukrani kwa Mbunge huyo kuona umuhimu wa kumsaidia mtoto huyo, huku akiongeza
kuwa msaada kama huo uendelee kutolewa kwa walemavu wengine pale panapojitokeza
fursa ya upatikanaji wa vifaa mbalimbali vya kusaidia watu wenye ulemavu.
No comments:
Post a Comment