Tangaza Biashara yako nasi kwa Matangazo ya aina mbalimbali, Mawasiliano zaidi piga simu namba 0762 578960
Monday, October 30, 2017
WASIMAMIZI MTIHANI KIDATO CHA NNE WAPEWA ONYO KALI
Katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania, Dokta Charles Msonde. |
Na Mwandishi wetu,
WAKATI Watahiniwa 385,938 wanatarajiwa kuanza mtihani wa
kumaliza kidato cha nne mwaka huu leo, Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetoa
onyo kali kwa wasimamizi wa mtihani huo.
Baraza hilo limesema kuwa halitasita kuchukua hatua kali
dhidi ya wasimamizi hao wa mitihani, pale itakapobainika kuna udanganyifu wa
aina yoyote ile.
Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dokta Charles Msonde alitoa
onyo hilo jana jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari ambapo alisema watahiniwa wa shule watakuwa 323,513 na wa kujitegemea
62,425.
Friday, October 27, 2017
BREAKING NEWS: KIKAO BARAZA LA MADIWANI MJI WA MBINGA CHAVUNJIKA MKURUGENZI MTENDAJI AKALIA KUTI KAVU AJIKUTA AKIWA KATIKA WAKATI MGUMU
Madiwani wa Halmashauri ya mji wa Mbinga na baadhi ya waalikwa wakitoka nje ya ukumbi baada ya kikao cha baraza la Madiwani hao kuvunjika. |
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, kikao cha baraza la
Madiwani wa Halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma, kimeshindwa kufanyika
na badala yake kimevunjika kufuatia Madiwani hao kumkataa Mkurugenzi mtendaji
wa halmashauri hiyo, Robert Kadaso Mageni wakidai kuwa hawataki kufanya naye
kazi tena kutokana na Mkurugenzi huyo kushindwa kusimamia kikamilifu miradi ya
maendeleo ya wananchi wa halmashauri hiyo.
Madiwani hao walichukua maamuzi hayo magumu leo katika kikao hicho
ambacho walitakiwa kupokea taarifa za maendeleo ya wananchi, robo ya kwanza ya
mwaka kilichoketi kwenye ukumbi wa Jumba la maendeleo uliopo mjini hapa.
Aidha maamuzi hayo yalifikiwa baada ya Mwenyekiti wa Madiwani
hao, Kipwele Ndunguru kufungua kikao cha baraza hilo na kuwataka Madiwake wake
wapokee agenda za kikao, ambapo kwa pamoja walimkatalia kupokea agenda hizo
huku wakieleza kuwa wapo tayari kuzipokea endapo Mkurugenzi huyo hatakuwepo
katika baraza hilo.
Thursday, October 26, 2017
WANANCHI MBINGA WAITAKA SERIKALI KUWAJIBISHA WAHUSIKA UPOTEVU WA MAPATO MSITU WA MBAMBI
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Dokta Binilith Mahenge. |
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
BAADA ya taarifa ya Kamati maalum iliyofanya kazi ya kuchunguza
uvunaji msitu wa Mbambi uliopo katika Halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani
Ruvuma, kuwasilisha taarifa ya kazi iliyofanya na kubaini hasara ya mapato ya
shilingi milioni 800 ambayo ilibidi yapatikane kutokana na uvunaji huo, baadhi
ya wananchi wamesema kuwa usimamizi wa kazi hiyo ungekuwa mzuri fedha hizo zingepatikana
na kuweza kuboresha huduma muhimu katika hospitali ya wilaya ya Mbinga iliyopo
mjini hapa.
Kadhalika walieleza kuwa hospitali hiyo ambayo hivi sasa
baadhi ya majengo yake ni chakavu likiwemo jengo la upasuaji ambalo halijafanyiwa
ukarabati kwa miaka mingi huku hali ya huduma ikiwa mbaya hivyo wanaiomba
serikali kuchukua hatua ili kuweza kunusuru hali hiyo.
“Hata dawa za kuhudumia akina mama wajawazito pale wanapofikia
hatua ya kujifungua wakati mwingine hazipatikani kwenye hii hospitali yetu na kusababisha baadhi yao
kupoteza maisha lakini fedha hizi zingepatikana zingeweza kuhudumia jamii”, walisema.
WOFMAIZE YASHINDA ZABUNI YA KUKUSANYA USHURU SONGEA
Na Albano Midelo,
Songea.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, imesaini
mkataba wa ukusanyaji ushuru wa mazao wa shilingi milioni 610 na kampuni ya
WOFMAIZE iliyopo hapa Songea.
Makubaliano ya kusaini mkataba huo yamekamilika Oktoba 24
mwaka huu katika Ofisi ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Abdul Hassan
Mshaweji huku yakishuhudiwa na wawakilishi wa kampuni hiyo pamoja na Kaimu
Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Songea Injinia Samwel Sanya.
Katika mikataba hiyo kampuni hiyo itahusika na ukusanyaji ushuru
wa mazao ya vyakula vilivyosindikwa na visivyosindikwa katika maeneo ya SODECO,
Manzese na maeneo mengine ya Manispaa hiyo.
KAYA MASKINI SONGEA WAWEZESHWA MILIONI 175
Baadhi ya wananchi waliopo kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini katika Manispaa ya Songea wakipata huduma. |
Na Albano Midelo,
Songea.
MFUKO wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Halmashauri ya
Manispaa ya Songea mkoani Euvuma, imeweza kuwasaidia wanufaika 4,881 waliopo kwenye
mpango wa kunusuru kaya maskini katika halmashauri hiyo kwa kuwapatia shilingi
milioni 175 ili ziweze kuwasaidia na hatimaye waweze kuondokana na umaskini.
Christopher Ngonyani ambaye ni Mratibu wa mfuko huo katika
halmashauri hiyo alimweleza mwandishi wetu kuwa fedha hizo zimetolewa katika
kipindi cha mwezi Septemba hadi Oktoba mwaka huu.
Alisema malipo hayo yamefanyika na kukamilika ndani ya wiki
hii katika mitaa 53 ambayo ina wanufaika hao.
Wednesday, October 25, 2017
SAKATA LA MSITU WA MBAMBI LAENDELEA KUMSAKAMA MKURUGENZI HALMASHAURI MJI WA MBINGA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli. |
Na Kassian
Nyandindi,
Mbinga.
SAKATA la tuhuma wizi wa mamilioni ya fedha za mradi wa uvunaji wa
msitu wa Mbambi katika Halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma, limeibua sura
mpya baada ya wananchi wa kata ya Matarawe mjini hapa kuitaka halmashauri hiyo
iwalipe asilimia 10 ya fedha za mapato yaliyotokana na msitu huo.
Asilimia hiyo ya mapato wanayodai wananchi hao imeelezwa kuwa
ni makubaliano yaliyofanywa katika vikao halali vilivyopita na kupitishwa na baraza
la Madiwani wa halmashauri ya mji huo.
Walisema wanamshangaa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya
mji wa Mbinga, Robert Kadaso Mageni kwa kutosimamia kikamilifu fedha za msitu
huo na kusababisha wizi huo ufanyike na wao kukosa sehemu ya mapato yao.
WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUWABANA MAFISADI
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
WANANCHI wa kijiji cha Lukalasi kitongoji cha Ngembambili
kijiji cha Mkako wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, wamempongeza Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli kwa kazi anayoendelea
kuifanya ya kuwaibua mafisadi na kuwachukulia hatua wakiwemo wezi wa madini.
Pongezi hizo zimetolewa hivi karibuni na wachimbaji wadogo wa
madini ambao wanaishi katika maeneo hayo mbele ya mkutano wa hadhara ambao
ulihudhuriwa na Mkuu wa mkoa huo, Dokta Binilith Mahenge.
Masha Mussa na Silvano Challe wakazi wa Ngembambili kwa nyakati
tofauti walisema kuwa kitendo anachokifanya Magufuli na kuwabana mafisadi hao
ambao walikuwa wanadhoofisha uchumi wa nchi, ni ujasiri wa hali ya juu hivyo
wamemwomba aendelee kukaza kamba zaidi ili kuweza kudhibiti vitendo hivyo viovu
visiweze kuendelea kutokea.
Tuesday, October 24, 2017
TFDA MANISPAA SONGEA YAKAMATA DAWA AMBAZO HAZIFAI KWA MATUMIZI YA BINADAMU
Mratibu wa Udhibiti wa Chakula na Dawa (TFDA) katika Manispaa ya Songea, Vitalis Mkomela akionesha dawa za aina mbalimbali kwa waandishi wa habari ambazo zimepita muda wake wa matumizi. |
Na Albano
Midelo,
Songea.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Chakula na Dawa (TFDA) katika Manispaa
ya Songea Mkoa wa Ruvuma, imekamata dawa za binadamu ambazo zilikuwa
zinaendelea kuuzwa zikiwa zimepita muda wake katika baadhi ya maduka ya dawa
muhimu yaliyopo mjini hapa.
Mratibu wa TFDA katika Manispaa hiyo, Vitalis Mkomela alisema
kuwa dawa za aina mbalimbali zenye thamani ya shilingi 244,000 zilikamatwa
katika operesheni maalum ambayo ilifanywa na watalaamu wa idara ya afya.
Mmiliki wa duka moja ambalo lilikutwa na dawa hizo amekiri
kuuza dawa hizo zilizomalizika muda wake na kwamba tayari amepigwa faini ya
shilingi 600,000.
Sunday, October 22, 2017
MKURUGENZI HALMASHAURI MJI WA MBINGA NA WENZAKE WATUHUMIWA KUTAFUNA MAMILIONI YA FEDHA ZA MSITU
Baraza maalum la Madiwani Halmashauri ya mji wa Mbinga likiwa limeketi katika kikao chake kujadili ubadhirifu wa fedha za mavuno ya msitu wa Mbambi katika halmashauri hiyo. |
Mwenyekiti wa Kamati maalum ya kuchunguza msitu wa Mbambi halmashauri mji wa Mbinga, Kelvin Mapunda akikabidhi taarifa ya uchunguzi kwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ndunguru Kipwele. |
Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani
Ruvuma, limetoa mapendekezo yake ya kumkataa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri
hiyo Robert Kadaso Mageni kwamba hawataki kufanya naye kazi tena, wakimtuhumu ametafuna
fedha za mauzo ya mbao zilizopasuliwa katika msitu wa Mbambi uliopo mjini hapa ambao
ni mali ya halmashauri ya mji huo.
Robert Kadaso Mageni. |
Aidha imeelezwa kuwa Mkurugenzi huyo amelipotosha baraza hilo
katika kikao walichoketi Novemba 2 hadi 3 mwaka jana na kutoa taarifa za uongo kwamba
msitu huo una jumla ya miti 5,4040 ambayo inafaa kupasuliwa mbao wakati ukweli
ni kwamba msitu ulikuwa na miti 8,470.
Kufuatia taarifa hizo ambazo hazikuwa sahihi wakati anazitoa
kwenye baraza hilo juu ya uvunaji wa msitu huo, hali hiyo imesababisha
halmashauri kupata hasara ya shilingi milioni 888,000,000.
Baada ya baraza hilo la Madiwani kutoa mapendekezo hayo ya
kumkataa, walimtaka Mkuu wa wilaya ya Mbinga, Cosmas Nshenye kufikisha kilio chao
kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli ili
aweze kuchukua hatua zaidi za kinidhamu dhidi ya mtumishi huyo.
SERIKALI YAPONGEZWA KWA KUBORESHA ELIMU KATIKA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VIKUU
Na Kassian Nyandindi,
Songea.
MJUMBE wa Kamati tendaji Taifa ya Chama Cha Walimu Tanzania
(CWT) mkoani Ruvuma, Sabina Lipukila ameipongeza Serikali ya awamu ya tano ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dokta John Pombe Magufuli
kwa kuona umuhimu wa kuboresha shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu hapa
nchini ikiwa ni lengo la kuhakikisha vijana wote wanapata elimu bora.
Hayo yalisemwa juzi na Mjumbe huyo katika mahafali ya tatu ya
kuhitimu wanafunzi wa kidato cha nne, katika sekondari ya kutwa ya Mahanje
iliyopo Madaba wilayani Songea mkoani hapa.
Alisema kuwa kufuatia hali hiyo wananchi wanapaswa kuunga
mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuboresha maendeleo ya sekta ya
elimu hapa nchini ili watoto wanaosoma katika shule hizo waweze kuwa katika
mazingira mazuri.
Wednesday, October 18, 2017
MANISPAA SONGEA YATOA MILIONI 49 KUWEZESHA WAJASIRIAMALI WAKE
Na Mwandishi wetu,
Songea.
IMEELEZWA kuwa Wajasiriamali wadogo wadogo waliopo katika
halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, watanufaika na mkopo wa
shilingi milioni 49 ambao umetolewa na halmashauri hiyo, kwa ajili ya kuwawezesha
wasonge mbele kimaendeleo katika shughuli zao za ujasiriamali.
Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii katika Manispaa hiyo,
Naftari Saiyoloi alitoa taarifa hiyo juzi mjini hapa, katika uzinduzi wa mfuko
wa vijana na wanawake.
Saiyoloi alibainisha kuwa shilingi milioni tisa zitakopeshwa
kwa vikundi kumi vya vijana na shilingi milioni 40 zitakopeshwa vikundi 39 vya
wanawake.
Sunday, October 15, 2017
WATU 2,458 MANISPAA SONGEA HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA
Mkuu wa wilaya ya Songea, Palolet Mgema akikagua zana za kufundishia katika Manispaa ya Songea. |
Na Albano Midelo,
Songea.
IMEELEZWA kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani
Ruvuma, ina Watu Wazima 2,458 ambao hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.
Afisa elimu ya Watu Wazima, Faraja Yonas alisema hayo juzi
ambapo alifafanua kuwa kati yao wanaume ni 661 na wanawake ni 1,797.
Yonas alibainisha kuwa kwa mujibu wa takwimu za usajili mwezi
Januari hadi Machi mwaka huu, Manispaa hiyo ina jumla ya Watu Wazima 119,328
ambapo kati yao wanaume ni 58,049 na wanawake ni 61,279.
Friday, October 13, 2017
TFDA SONGEA YAKAMATA MAFUTA FEKI YA ALBINO NA VYAKULA VILIVYOHARIBIKA
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Songea, Mameritha Basike akionesha kwa waandishi wa habari mafuta feki ya Albino ambayo yalikamatwa katika moja ya duka linalouza vipodozi mjini hapa. |
Baadhi ya vyakula vilivyoharibika na mafuta feki ya albino ambavyo vilikamatwa hivi karibuni na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Songea. |
Na Albano Midelo,
Songea.
IDARA ya Afya katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, kwa
kushirikiana na watalaamu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wamefanya Operesheni katika maduka ya vipodozi katika mji wa Songea mkoani humo na
kufanikiwa kukamata mafuta ya Albino yakiuzwa kinyume cha sheria na taratibu
husika.
Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dokta Mameritha Basike alisema
mafuta hayo yalikamatwa juzi katika duka la Godluck Mranga ambayo yalikuwa yanauzwa
shilingi 4,500.
“Hairuhusiwi mafuta ya kupaka Albino aina ya Sunblock Cream
UV40 kuwepo kwenye maduka ya vipodozi badala yake mafuta haya yanaruhusiwa
kuwepo kwenye maduka ya dawa (Pharmacy)”, alisema Dokta Basike.
MANISPAA SONGEA YAVUNJA MKATABA NA MKANDARASI
Hii ni moja kati ya sehemu ya barabara mtaa wa FFU kwenda Matogoro yenye urefu wa kilometa 3.2 inayojengwa kwa kiwango cha lami nzito katika Manispaa ya Songea. |
Na Mwandishi wetu,
Songea
HATIMAYE Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,
imevunja rasmi Mkataba ujenzi wa lami nzito kati yake na Kampuni ya Lukolo
yenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo, Mhandisi
Samwel Sanya alisema kuwa wamechukua maamuzi hayo baada ya muda wa Mkataba wa
kumaliza kazi kwa Mkandarasi huyo ulimalizika tangu Juni 30 mwaka huu.
Alisema kuwa baada ya muda huo kumalizika Mkandarasi huyo
aliingizwa kwenye tozo (Liquidated Damage) na kwamba iwapo atashindwa kumaliza
kazi kwa siku 100 hatua za kisheria za kuvunja mkataba zitafanyika.
Thursday, October 12, 2017
MWANSASU MWENYEKITI MPYA WA CHAMA CHA MAPINDUZI NAMTUMBO
Na Yeremias Ngerangera,
Namtumbo.
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Namtumbo mkoa
wa Ruvuma wamemchagua, Aggrey Mwansasu kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM wilayani
humo baada ya kumbwaga chini aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Benjamini
Nindi.
Uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti huyo ulifanyika juzi kwenye
ukumbi wa shule ya Sekondari Namtumbo, ambayo inamilikiwa na Jumuiya ya wazazi ya
Chama Cha Mapinduzi iliyopo mjini hapa.
Katika uchaguzi huo awali uliingia dosari baada ya msimamizi
wa uchaguzi huo, Zena Mijinga kujisahau kwa kutosoma kanuni ya ushindi wa uchaguzi
huo ambapo mgombea ni sharti apate kura zaidi ya nusu ya wapiga kura waliopo
kwenye uchaguzi huo.
FUMANIZI LADAIWA KUSABABISHA GARI KUTEKETEZWA MOTO
Gari aina ya Noah linalodaiwa kuteketea kwa moto eneo la Peramiho wilayani Songea baada ya fumanizi. |
Na Albano Midelo,
Songea.
GARI aina ya Noah limeteketea kwa moto katika eneo la
Peramiho wilayani Songea mkoa wa Ruvuma.
Taarifa za awali za mashuhuda waliohojiwa katika eneo la
tukio walidai kuwa gari hilo liliteketezwa, kutokana na sababu za fumanizi la
mke wa mtu ambaye inadaiwa kuwa mwenye mume aliamua kuteketeza gari hilo.
Uchunguzi umebaini kwamba ubavuni mwa gari hilo ambalo
limeteketea yameandikwa maneno kwa rangi nyeusi, kuwa mke wa mtu ni sumu ambapo
akinamama wanne waliokutwa katika eneo hilo walidai kuwa tukio hilo
lilisababishwa na fumanizi.
WANANCHI MITENDEWAWA NA CHANDARUA SONGEA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA
Na Albano Midelo,
Songea.
MTAA wa Mitendewawa na Chandarua iliyopo katika Manispaa ya
Songea mkoani Ruvuma, wananchi wake wanatarajia kunufaika na kuondokana na adha ya upatikanaji wa maji safi na salama, baada ya serikali
kuanza kujenga mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 517.
Samwel Sanya ambaye ni Mhandisi wa Maji katika Manispaa hiyo alisema
hayo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Songea, Palolet Mgema wakati Mkuu huyo wa
wilaya alipofanya ziara yake ya ukaguzi wa mradi huo.
Alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo ulitakiwa kuanza mwaka
wa fedha wa 2014/2015 lakini utekelezaji wake haukufanikiwa kutokana na fedha
hizo kuchelewa kuwafikia kutoka Serikali kuu.
Sunday, October 8, 2017
MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA MAHAFALI DARASA LA SABA DE PAUL SONGEA
Wahitimu wa darasa la saba shule ya De Paul Msamala wakionesha umahili wao wa kucheza muziki wakati wa mahafali yao ya kumaliza elimu ya msingi shuleni hapo. |
NAMSWEA MBINGA WAFANYA TAMASHA LA MICHEZO KUHAMASISHA MAENDELEO
Washiriki wa mchezo, mpira wa miguu wakiwa katika picha ya pamoja siku ya tukio la tamasha la michezo katika tarafa ya Namswea wilayani Mbinga. |
Na Mwandishi wetu,
Mbinga.
KATIKA kuenzi utamaduni wa
kiafrika, Wananchi wanaoishi katika tarafa ya Namswea wilaya ya Mbinga mkoani
Ruvuma wamefanya tamasha la michezo mchanganyiko ndani ya tarafa hiyo, ikiwa ni
lengo la kuhamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo.
Tamasha hilo lilizinduliwa
hivi karibuni katika viwanja vya michezo Namswea likiwa limebeba kauli mbiu “Ujana ni hazina tuutumie vizuri kwa
manufaa ya sasa na baadae” ambapo lilifadhiliwa na Thotnant Ezekiel Kayombo
ambaye alikuwa mgeni rasmi huku michezo iliyokuwa ikichezwa siku hiyo ni
mpira wa miguu na ngoma mbalimbali za asili.
Akizungumza na mwandishi
wetu, Kayombo alifafanua kuwa lengo la tamasha hilo ni kufikisha ujumbe huo kwa
jamii hasa vijana juu ya wajibu wao katika kushiriki kwenye shughuli za
kimaendeleo katika maeneo yao wanayoishi.
Saturday, October 7, 2017
MANISPAA SONGEA YAFAULISHA KIDATO CHA SITA KWA ASILIMIA 97
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Abdul Hassan Mshaweji. |
Na Albano Midelo,
Songea.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imeendelea
kufanya vizuri katika mtihani wa Taifa kidato cha sita, baada ya kufaulisha kwa
asilimia 97.2.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, shule tano za Serikali kidato cha
sita wanafunzi ambao walipata daraja la kwanza ni 62 na kwamba kati yao
wavulana ni 34 na wasichana ni 28.
Daraja la pili lina jumla ya wanafunzi 471 kati yao wavulana
ni 174 na wasichana 297 ambapo daraja la tatu wapo jumla ya wanafunzi 507 kati
yao wavulana ni 179 na wasichana 328.
Friday, October 6, 2017
WATUMISHI SONGEA WAPATA MAFUNZO YA KUANDAA BAJETI KWA MFUMO WA MTANDAO
Christopher Ngonyani mwezeshaji wa mafunzo ya kuandaa bajeti kwa mfumo wa mtandao akitoa elimu kwa watumishi wa halmashauri ya Manispaa ya Songea namna ya kutumia mfumo huo. |
Watumishi wakiwa katika mafunzo ya mfumo wa kuandaa bajeti kwa njia ya kieletroniki. |
Na Kassian Nyandindi,
Songea.
WATUMISHI 49 waliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea
mkoani Ruvuma, wamepata mafunzo ya siku tano ya Mfumo wa kieletroniki ambayo
yatapunguza gharama za uendeshaji katika maandalizi, uwasilishaji na
utekelezaji wa mipango ya bajeti mpya katika shughuli mbalimbali za halmashauri.
Mafunzo hayo yamefunguliwa juzi na Kaimu Mkurugenzi wa
halmashauri ya Manispaa hiyo, Injinia Samwel Sanya katika ukumbi wa halmashauri
hiyo uliopo mjini hapa.
Christopher Ngonyani ambaye ndiye mwezeshaji wa mafunzo hayo
alisema kuwa mfumo huo mpya ambao umeanza kutumika rasmi hapa nchini kuanzia
mwezi Septemba mwaka huu, utaweza kupunguza gharama za safari kwa Wakuu wa idara
na wahasibu ndani ya halmashauri zote hapa nchini.
MILIONI 127 KUTUMIKA UJENZI WA DARAJA MATARAWE SONGEA
Upande wa kushoto, Mkuu wa wilaya ya Songea Palolet Mgema akitoa msisitizo juu ya ujenzi wa daraja la Matarawe alipofanya ziara yake juzi. |
Na Mwandishi wetu,
Songea.
MKUU wa Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma, Palolet Kamando Mgema
amefanya ziara ya kushitukiza kukagua ujenzi wa daraja la mto Matarawe lililopo
katika Manispaa ya Songea mkoani humo.
Ziara hiyo imefanyika juzi ambapo daraja hilo limekuwa ni kiungo
muhimu kwa wananchi wa Kata ya Matarawe, Mjimwema na kata nyingine jirani mjini
hapa.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Injinia Samwel Sanya alisema
kuwa zaidi ya shilingi milioni 127 zimetengwa kwa ajili ya kazi ya kukamilisha ujenzi
wa daraja hilo.
OFISI YA KATA MJIMWEMA SONGEA YAGHARIMU UJENZI WAKE MILIONI 25.5
Ofisi ya kata Mjimwema Songea. |
Na Albano Midelo,
Songea.
MRADI wa ujenzi Ofisi ya Kata Mjimwema iliyopo katika Halmashauri
ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma umegharimu shilingi milioni 25.56 ambapo
ujenzi huo umetokana na fedha zilizotolewa na michango ya wananchi na serikali.
Afisa Mtendaji wa kata hiyo, Stan Kibiki alisema kuwa kati ya
fedha hizo nguvu ya wananchi ni shilingi 556,000 na gharama ya serikali ni shilingi
milioni 25.
Vilevile alisema mradi wa ujenzi ya ofisi hiyo ulianza tangu
mwaka wa fedha wa 2012/2013 ambapo amezitaja shughuli ambazo zilifanyika katika
kipindi hicho kuwa ni pamoja na kusafisha eneo la mradi, kujenga msingi na
kunyanyua ujenzi wa jengo husika.
Wednesday, October 4, 2017
WIZARA YA AFYA YATOA TAHADHARI UWEPO UGONJWA WA TAUNI MADAGASCAR
Imeelezwa kuwa kati ya wagonjwa 104 walioripotiwa, 20
wamefariki dunia, ambapo taarifa iliyotolewa jana Jumanne na Ofisa Habari wa Wizara
hiyo, Catherine Sungura imesema kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) limeeleza
nchini Madagascar mikoa minane imeripotiwa kuwepo wagonjwa ukiwemo mji
mkuu wa nchi hiyo, Antananarivo.
Ugonjwa huo ulianza kuripotiwa Agosti 23 hadi Septemba 28
mwaka huu.
“Wengi walioripotiwa wameonyesha kuwa na uhusiano kwa njia
moja au nyingine na mgonjwa wa kwanza jambo linalothibitisha yapo maambukizi ya
ugonjwa wa tauni kati ya binadamu na binadamu.
Hivyo kwa mujibu wa WHO, ipo hatari ya wastani (Moderate
risk) ya ugonjwa huo kusambaa katika nchi jirani na Madagascar,” imesema
taarifa hiyo.
VITUO VYA ELIMU VISIVYOSAJILIWA SONGEA MARUFUKU KUTOA HUDUMA
Ofisi za Halmashauri Manispaa ya Songea. |
Na Albano Midelo,
Songea.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani hapa, imewaandikia
barua wamiliki wote wa vituo vya kutolea elimu yoyote bila kusajiliwa kuacha
mara moja tabia hiyo, kwa kuwa ni kinyume cha sheria za nchi na endapo kutakuwa
na mtu anafanya hivyo atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufikishwa Mahakamani.
Idara ya elimu katika Manispaa hiyo imetoa agizo hilo juzi kwa Waratibu
elimu kata wote waliopo kwenye Manispaa ya Songea kusimamia ipasavyo utekelezaji wake ambapo kuanzia mwezi
uliopita Septemba mwaka huu imepigwa marufuku hairuhusiwi mmiliki wa shule au
kituo chochote kile cha kutolea mafunzo ya tuition kutoa masomo bila kusajiliwa.
Imebainisha kuwa kumeibuka taasisi zisizokuwa rasmi na watu
binafsi kuanzisha vituo vya elimu na kujitangaza kwa njia mbalimbali kwamba
wanatoa masomo ya ngazi mbalimbali ya elimu kuanzia elimu ya chekechea, msingi,
sekondari na vyuo.
WAZEE MANISPAA SONGEA WALIA NA MATIBABU
Eliezer Nyoni Mwenyekiti Baraza huru la wazee Manispaa ya Songea. |
Na Albano Midelo,
Songea.
WAZEE katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma
wameiomba Serikali kutatua kero ya kupata matibabu bure, ambayo inaongoza kwa
wazee wa Manispaa hiyo hali ambayo inasababisha wengi wao kukosa matibabu.
Akisoma risala ya maadhimisho ya siku ya wazee duniani Oktoba
Mosi mwaka huu, Makamu Mwenyekiti wa Baraza Huru la Wazee wa Manispaa ya Songea
Sophia Hasara, alisema ni muhimu sasa kwa Serikali kuwapatia wazee hao kadi za
matibabu bure kama ilivyoelekezwa hapo awali ili waweze kuondokana na kero hiyo
pale wanapokwenda kupatiwa matibabu katika vituo vya serikali.
Hasara alisema kuwa kuna umuhimu kwa Manispaa hiyo kuharakisha
mchakato wa upatikanaji wa kadi hizo kwa wazee wote ili kuweza kumaliza kero
hiyo ambayo imedumu kwa muda mrefu na sasa inasababisha baadhi ya wazee
kupoteza maisha kutokana na wakati mwingine wanashindwa kugharamia matibabu.
Monday, October 2, 2017
SHEIKH PONDA AINGILIA KATI SAKATA LA WATU WASIOJULIKANA
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh
Ponda Issa Ponda amemkosoa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI),
Robert Boaz akieleza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimeshindwa kuchunguza
matukio ya uhalifu yanayotokea nchini.
Akiwa nchini China kuhudhuria mkutano mkuu wa 86 wa Taasisi
ya Polisi ya Kimataifa (Interpol), Boaz alikaririwa na gazeti moja la Serikali
akisema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vina uwezo wa kuchunguza matukio ya
uhalifu, yakiwamo mauaji na utekaji bila kusaidiwa na vyombo vya nje.
Hata hivyo, Sheikh Ponda aliyempigia simu jana mwandishi
wetu, alisema kauli iliyotolewa na DCI haina ukweli.
WADAU MBINGA WATAKIWA KUCHANGIA MAENDELEO SHULE YA SEKONDARI MKINGA
Na Mwandishi maalum,
Mbinga.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM)
wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, Sostenes Nchimbi amewaomba Wadau mbalimbali
waliopo wilayani humo kujitokeza kwa wingi na kuchangia maendeleo ya shule ya sekondari
ya wazazi Mkinga iliyopo katika wilaya hiyo.
Ombi hilo lilitolewa juzi na Mwenyekiti huyo wakati alipokuwa
ametembelea shule hiyo huku akiwa ameambatana na viongozi wengine wa jumuiya
hiyo kwa lengo la kujionea maendeleo yake na changamoto mbalimbali.
“Tumeingia madarakani kwa lengo la kuweza kuisaidia jamii
iweze kusonga mbele kimaendeleo siku zote umoja ni nguvu utengano ni udhaifu,
napenda kueleza kwamba nipo tayari kuunga mkono katika maendeleo ya shule hii”,
alisema Nchimbi.
Subscribe to:
Posts (Atom)