Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
MTUHUMIWA ambaye alikuwa akishikiliwa katika Kituo kikuu cha
Polisi wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Bosco Ndunguru (40) amekutwa akiwa
amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia shati ambalo alikuwa amelivaa,
wakati alipokuwa kwenye mahabusu ya kituo hicho cha polisi wilayani humo.
Ndunguru aliwekwa mahabusu, kwa tuhuma ya kuvunja jengo la
polisi na kuiba Radio call ya kituo hicho mwaka jana, ambapo alitoroka
kusikojulikana na Jeshi hilo lilikuwa likimtafuta kwa muda mrefu.
Taarifa zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea Januari 23 mwaka
huu majira ya asubuhi, ambapo baada ya kukamatwa na kuswekwa rumande ilikuwa afikishwe
Mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma, ambazo zilikuwa zinamkabili.
Imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kuingizwa mahabusu,
muda mwingi alikuwa akilia na kulalamika sana, huku akidai kuwa ndugu zake
hawampendi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela alisema mara
baada ya askari waliokuwa zamu kumaliza muda wao na kuingia wengine na kabla ya
kutoka kazini, askari hao walikabidhiana kituo pamoja na mali zilizopo kituoni
hapo ambapo mtuhumiwa huyo pamoja na watuhumiwa wengine watatu wenye makosa tofauti
wakiwa katika mahabusu hiyo, ndipo Bosco alitumia muda huo kutoka na kujifanya
akielekea chooni na kuingia chumba kilichopo jirani na mahabusu ambacho
kilikuwa hakina mtu na kuchukua uamuzi wa kujitundika kwa kutumia shati hilo
ambalo alikuwa amevaa.
Alisema aliweza kufanikisha tendo hilo la kujitundika kwenye nondo ya mlango wa chumba hicho, mpaka alipogunduliwa na mmoja kati ya watuhumiwa waliokuwepo ndani na kutoa taarifa kwa askari waliokuwa zamu, siku ya pili Januari 24 mwaka huu majira ya saa moja asubuhi.
Kamanda huyo aliongeza kuwa mwili wa marehemu huyo, ulifanyiwa uchunguzi na mganga kutoka hospitali ya wilaya ya Mbinga, ambapo baada ya kukamilisha kazi hiyo ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

No comments:
Post a Comment