Na Mwandishi
wetu,
Tunduru.
AWEZAE Mohamed (35) amefariki dunia kufuatia ajali mbaya
iliyotokana na pikipiki ambayo alikuwa akisafiria, kugongwa na
lori aina ya Steya lenye namba za usajili T 862BFW ambalo linatumiwa kubeba
kifusi cha udongo.
Kadhalika mume wake Issa Swalehe naye amelazwa katika
Hospitali ya wilaya ya Tunduru kufuatia ajali hiyo, ambaye ni mlinzi katika
kampuni ya kichina ambayo inajenga barabara kutoka Tunduru mjini hadi kata ya Matemanga
wilayani humo.
Tukio hilo lilitokea Aprili 3 mwaka huu, kijiji cha Amani
katika kata ya Nandembo wilayani humo ambapo marehemu huyo alikuwa akisafiria
pikipiki aina ya Sunlg yenye namba za usajili T 886 CTC ambayo ilikuwa
ikiendeshwa na mumewe huyo.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma, Revocatus Malimi
alisema chanzo cha ajali hiyo, bado hakijafahamika na kwamba dereva wa lori
hilo Rashid Shaban ametokomea kusikojulikana na polisi bado wanamtafuta.
Akizungumza kwa shida, majeruhi Ngulinga ambaye amelazwa wodi
namba tatu katika hospitali ya wilaya hiyo alisema, chanzo cha ajali hiyo ni
uzembe uliofanywa na dereva wa lori hilo, baada ya kuwaruhusu wapite ndipo
waligongana.
No comments:
Post a Comment