Na Mwandishi wetu,
Songea.
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mkazi mmoja ambaye anaishi wa
mtaa wa Mateka kata ya Mateka Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Denis Komba (26)
amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa Songea mkoa hapa, baada ya watu wenye
hasira kumuua kwa mawe na fimbo nyoka aliyekuwa amembeba kwenye mfuko wa
jaketi.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Komba kabla ya
kufariki dunia alikuwa amekodi pikipi ya Kassian Haulle (24) mkazi wa Mpitimbi yenye
namba za usajili MC 724 AKB aina ya Sunlg, ili apelekwe nyumbani kwake anakoishi
Mateka.
Zubery Mwombeji. |
Aidha walipofika eneo ilipokuwa zamani Benki ya Posta mjini
hapa barabara kuu ya Sokoine, dereva wa pikipiki alianza kuhisi kwamba kuna
kitu kinamtekenya na kumgonga gonga sehemu ya mgongoni na kwamba alipogeuka
nyuma ili aweze kujua nini, ndipo alimuona nyoka mkubwa amesimamisha kichwa huku
akiwa amebebwa na mteja huyo aliyekodi pikipiki yake.
Kwa upande wake Haulle alisema kuwa, mara baada ya kumuona
nyoka huyo alilazimika kuruka kutoka kwenye pikipiki hiyo ambapo baada
ya kuanguka nyoka huyo alikimbilia kwenye Kalavati la maji machafu lililopo
kando kando ya barabara na kuanza kupiga kelele za kuomba msaada ndipo kundi la
vijana wenzake ambao ni waendesha pikipiki walijitokeza na kuwasili katika eneo
la tukio hilo kwa lengo la kumsaidia mwenzao.
Kabla ya vijana hao hawafanya jambo lolote marehemu Komba ambaye
alikuwa amembeba nyoka huyo, aliwaomba vijana hao na watu wengine waliofika
katika eneo hilo la tukio wasimpige nyoka wake, kwani iwapo watampiga na kufa
yeye pia atapoteza maisha.
Kufuatia maneno hayo, Haulle alimtoa nyoka huyo ndani ya
Kalavati kwa kushirikiana na vijana wenzake walianza kumpiga hadi kufa na ndipo
marehemu Komba alipoona nyoka wake anapigwa, alianza kulegea na kuanguka chini
ghafla huku akitokwa povu mdomoni na puani.
Habari zinasema kuwa, baada ya Komba kuanguka na kuwa katika
hali mbaya alikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu
hata hivyo, juhudi za madaktari na wauguzi wa hospitali ya Rufaa Songea za
kuokoa maisha yake zilishindikana na hatimaye alifariki dunia.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Zubery Mwombeji
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu haukuwa
na jeraha lolote na ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti, katika
hospitali hiyo na nyoka aliyeuawa amechukuliwa na idara ya maliasili kwa uchunguzi zaidi
juu ya tukio hilo ili kuweza kubaini kiini na chanzo cha tukio hilo.
Mwombeji alifafanua kuwa kwa upande wa dereva wa pikipiki yeye
anaendelea vizuri na anapatiwa matibabu katika hospitali hiyo ya Rufaa.
Vilevile alisema kuwa ametoa rai kwa wananchi kuacha tabia ya
kujichukulia sheria mkononi, huku akiwataka waache kumiliki nyara za serikali
zinazoweza kuwaletea madhara kama vile majeraha au vifo.
Katika tukio jingine mkazi mmoja wa kijiji cha
Mdunduwalo, Joseph Charles (27)amefariki dunia kwa kuchomwa na
kitu chenye ncha kali tumboni na mtu aliyefahamika kwa jina la Oddo Komba (34)
ambaye ni mkazi wa Mhepai Peramiho baada ya kuhitilafiana wakati wakitoka
kunywa pombe za kienyeji.
Kamanda huyo wa Polisi alieleza kuwa tukio hilo lilitokea Disemba
26 mwaka huu majira ya saa moja usiku katika kijiji cha Mtyangimbole kata ya
Gumbiro halmashauri ya wilaya ya Madaba wilayani Songea mkoani humo, ambapo
chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi uliotokea njiani kati yao wakati wakiwa wanarudi
nyumbani kutoka kwenye klabu zinazouza pombe za kienyeji.
No comments:
Post a Comment