Na Mwandishi wetu,
Songea.
KATIKA kuendeleza miradi ya maji safi na usafi wa mazingira,
serikali hapa nchini imetoa zaidi ya shilingi milioni 55 kwa halmashauri ya
Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, kwa ajili ya kuendeleza miradi hiyo kwa
manufaa ya wananchi wake.
Aidha imefafanuliwa kuwa fedha hizo zitatumika kwa ajili ya
utekelezaji wa mradi wa maji na usafi wa mazingira kwa lengo la kuzijengea
uwezo Jumuiya za Watumiaji Maji (COWSO) na usimamizi wa maji.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Ofisa habari wa
Manispaa hiyo, Albano Midelo alisema kuwa fedha hizo tayari zimetumika katika
suala la uchangiaji huduma ya matumizi ya maji katika mitaa ya Mahilo, Muhombezi,
Ruhuwiko Kanisani na Chandarua.
Mkoa wa Ruvuma unakadiriwa kuwa na
wakazi 1,497,853 kati ya hao wakazi 851,034 sawa na asilimia 57 tu, ndiyo
wanaopata maji safi na salama kwa mujibu wa takwimu za kufikia mwishoni mwa
mwezi Oktoba mwaka huu.
Midelo aliongeza kuwa katika maeneo
ya vijijni wakazi wanaopata huduma ya maji safi na salama ni asilimia 54.4 huku
kwa wale wanaoishi mjini hupata kwa asilimia 68.1.
No comments:
Post a Comment