Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC)
Deo Nsokolo akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya hukumu ya kesi
hiyo.
|
Jinsi mauaji yalivyofanyika. |
IRINGA:
MAHAKAMA kuu ya Tanzania kanda ya
Iringa, leo imemuhukumu kwenda jela miaka 15 askari wa Kikosi
cha Kutuliza Ghasia (FFU) mwenye namba G. 2573 Pacificius Cleophace
Simon (27) aliyemuua mwandishi wa habari wa
kituo cha Chanel Ten, Daudi Mwangosi.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji wa Mahakama hiyo Dkt. Paul Kihwelo
alisema kuwa mshtakiwa huyo amekutwa na hatia ya kuua bila kukusudia katika
shitaka la pili lililosomwa Mahakamani hapo leo, baada ya la kwanza kusomwa na
kukutwa hana hatia.
Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mwezi Februari 12, mwaka 2012
na kufikia hukumu hiyo ya kumtia hatiani na kwamba tukio hilo lilitokea
Septemba 2 mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo, wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa.
No comments:
Post a Comment