Na Julius Konala,
Songea.
SERIKALI mkoani Ruvuma imewasimamisha kazi watumishi nane
kutoka halmashauri za wilaya nne za mkoa huo ikiwemo katika wilaya zake za Tunduru,
Nyasa, Mbinga na Namtumbo kwa lengo la kupisha uchunguzi baada ya kubainika
wameshindwa kuzingatia weledi wa utumishi wa umma ikiwemo kufanya vitendo vya
ubadhirifu wa fedha.
Hayo yalisemwa na Katibu tawala wa mkoa huo, Hassan Bendeyeko
alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa mipango
uliopo kwenye Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma.
Bendeyeko aliwataja watumishi waliosimamishwa kazi kuwa ni Fortunatus
Mlokozi Kakiko, ambaye ni mkaguzi wa ndani Alan Ansigali Mbunda ni Afisa ugavi
na Juma Kassim Kasalo ambaye ni Mweka Hazina wote wanatoka halmashauri ya
wilaya ya Tunduru.
Wengine ni Joseph Ngonyani ni mweka Hazina na Nelson Kiwehuru
ambaye ni mkaguzi wa ndani wote wa kutoka halmashauri ya wilaya ya Nyasa, na
kwamba Klodwick Mapunda (Mweka Hazina), Robert Mahili (Mkaguzi wa kitengo cha
manunuzi) toka halmashauri ya wilaya ya Namtumbo pamoja na Emmanuel Kapinga
ambaye Afisa utumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga.
Katibu tawala huyo aliwataja watumishi wanaokwenda kuziba nafasi
zilizoachwa wazi kwenye halmashauri hizo kuwa ni Emmanuel Nyomeye (CPA Holder) kutoka
Mbinga mji na kuwa mweka hazina wilaya ya Tunduru, Paulo Humba toka Sekretarieti
ya mkoa na kuwa mkuu wa kitengo cha manunuzi wilaya ya Tunduru huku Abubakari
Shayo toka Namtumbo anaenda kuwa mkaguzi wa ndani wilaya ya Tunduru.
Aliendelea kuwataja wengine kuwa ni Willy Luambano kutoka
Namtumbo anaenda kuwa mkaguzi wa ndani halmashauri ya wilaya ya Nyasa, Pendo
Nyomeye kutoka Tunduru anakwenda kufanya kazi ya kuwa mweka hazina wilaya ya Nyasa,
Marcela Mapunda kutoka Tunduru kuwa, Afisa manunuzi wilaya Namtumbo, Peter
Tumaini kutoka Manispaa ya Songea anaenda kuwa mweka hazina wilaya Namtumbo na
Leokadia Humera kutoka Tunduru anaenda kuwa Afisa utumishi mwandamizi wilaya ya
Mbinga.
Kufuatia kutokea kwa matatizo hayo, Katibu tawala wa mkoa wa
Ruvuma, Bendeyeko alisema kuwa serikali imeunda kamati ya uchunguzi
itakayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhandisi Ezla Daniel wa kutoka Wakala wa barabara
Tanzania mkoani humo (TANROADS), Nelson Kailembo (PCCB) Norbetha Nyoni (Mkuu wa
idara ya utumishi Madaba) na Adelina Komba kutoka ofisi ya Katibu tawala wa
mkoa huo ambapo amedai kuwa yeyote atakayebainika kufanya makosa kwenye
uchunguzi huo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
No comments:
Post a Comment