KAMPUNI ya uchimbaji madini ya Acacia, imezikataa taarifa
zote zilizotolewa katika ripoti ya Kamati ya pili iliyochunguza Makontena 277
ya mchanga wa madini yaliyozuiwa.
Acacia wamesema hayo ikiwa ni siku moja tu, baada ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kupokea ripoti ya Kamati ya pili
ya Wanasheria na Wachumi waliochunguza sakata hilo la mchanga wa madini.
Pia kampuni hiyo imetaka uchunguzi huru wa ripoti ya Kamati
ya kwanza na ya pili zilizoundwa na Rais Magufuli kuchunguza mchanga huo.
“Migodi yetu inafanya kazi kihalali kwa kufuata sheria za
Tanzania, hata usafirishaji wa mchanga huu unafanywa kwa kufuata sheria na
kupata kibali cha usafirishaji,” imesema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa zuio la kusafirishwa mchanga huo
haliiathiri Acacia pekee bali hata maisha ya maelfu ya Watanzania zaidi ya
36,200.
“Kampuni hii imekuwa ikiwekeza katika elimu, miundombinu na
miradi ya afya na hivi vyote vitaathirika wakati zuio hili likiendelea”, imesema.
No comments:
Post a Comment