Washiriki kutoka sekta mbalimbali wakishuhudia uzinduzi wa shughuli za Chuo Kikuu Cha Kilimo (SUA) ambazo zimefanyika leo Songea mjini mkoani Ruvuma. |
Na Mwandishi wetu,
Songea.
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Dkt. Binilith Mahenge amezindua shughuli za Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) mkoani Ruvuma, ambazo zinatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa baada ya taratibu husika kukamilika.
Uzinduzi huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea uliopo mjini hapa ambapo ulishirikisha mwakilishi wa Mkuu wa chuo hicho, Profesa Peter Gillah.
Vilevile kulikuwa na Mkuu wa ndaki ya misitu, wanyamapori na utalii Profesa John Kessy.
Wakuu wa wilaya ya Mbinga, Tunduru, Nyasa na wakurugenzi wa halmashauri mkoa wa Ruvuma, wakuu wa idara na vitengo pamoja na wataalamu mbalimbali wa maliasili na utalii mkoani humo.
Wakuu wa wilaya ya Mbinga, Tunduru, Nyasa na wakurugenzi wa halmashauri mkoa wa Ruvuma, wakuu wa idara na vitengo pamoja na wataalamu mbalimbali wa maliasili na utalii mkoani humo.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo profesa Gillah ambaye alimwakilisha Mkuu wa Chuo Kikuu cha SUA, amemshukuru Mkuu wa mkoa huyo Dkt. Mahenge kwa kuwapokea ili kufungua Chuo kikuu tawi la SUA nyanda za juu kusini mkoani hapa.
Majengo ya SUA yanatarajiwa kujengwa katika mtaa wa Masigira kata ya Tanga Manispaa ya Songea ambapo wananchi wa maeneo hayo mpaka sasa, wametoa eneo lenye ukubwa wa ekari 40 na kwamba jitihada za kutafuta maeneo mengine katika wilaya zingine zilizopo mkoani humo zinaendelea ili kuweza kufikia malengo husika.
No comments:
Post a Comment