SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai
amewakumbusha Wabunge wa upinzani wanaotaka marais wastaafu washtakiwe kuhusu
sakata la mchanga wa madini, akiwaeleza kuwa wanapaswa wakumbuke pia wanao
mawaziri wakuu wastaafu wawili ambao nao watahusika pia.
Job Ndugai. |
Ndugai alisema hayo leo Bungeni baada ya mchango wa Mbunge wa
Kilombero, Peter Lijualikali akisema kuwa haiwezekani Mawaziri na watendaji
wengine wa Serikali wakafanikisha mikataba mibovu ya madini bila ridhaa ya
Rais.
“Haiwezekani mzee wangu (Andrew) Chenge
na (Nazir) Karamagi walipitisha mikataba hiyo bila Rais aliyekuwapo kufahamu, Kinga
ya Rais kushtakiwa iondolewe ili wahojiwe”, alisema Lijualikali.
Baada ya Mbunge huyo kutoa hoja hiyo ambayo inafanana na ya
Mbunge wa Tarime vijijini, John Heche, Spika wa Bunge Ndugai aliwakumbusha juu
ya mawaziri wastaafu walionao kwenye chama chao.
“Mabadiliko mnayoyataka yakipitishwa
na viongozi mlionao wakikamatwa msije mkalalamika tena”, alisema Ndugai.
No comments:
Post a Comment