Na Steven Augustino,
Tunduru.
ALLY Mchumwa (45) ambaye ni mtuhumiwa wa tukio la mauaji ya
Shekhe wa Msikiti wa kijiji cha Likweso, wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma
amefikishwa katika Mahakama ya wilaya hiyo kujibu tuhuma zinazomkabili juu ya
tukio hilo.
Habari zinaeleza kuwa, kabla ya mtuhumiwa huyo kutekeleza
unyama huo alimuua kwa kumchoma kisu shingoni Shekhe, Seleman Mwarabu Selemani (45)
katika tukio la fumanizi lililotokea Mei 22 mwaka huu.
Akimsomea shauri hilo la mauaji namba 4/2016 mbele ya Hakimu
mfawidhi wa Mahakama ya wilaya hiyo, Gladys Barthy mwendesha mashtaka mkaguzi msaidizi
wa Polisi Inspekta Songelaeli Jwagu alisema kuwa, tukio hilo lilitokea
siku hiyo majira ya saa 3.30 asubuhi katika eneo la mashamba ya
Mkasandimbe yaliyopo tarafa ya Nakapanya, wilayani Tunduru.
Inspekta Jwagu alidai Mahakamani hapo kuwa, kitendo
alichokifanya mtuhumiwa Ally ni kosa kinyume cha sheria namba 196 cha sheria ya
kanuni ya adhabu sura namba 16, kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Pamoja na mambo mengine, kutokana na Mahakama hiyo haina
mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji mtuhumiwa huyo, hakutakiwa kujibu chochote
Mahakamani hapo na kwamba shauri hilo litatajwa tena Juni 4 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment