Na Kassian
Nyandindi,
Mbinga.
MKUU wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Cosmas Nshenye
amesema kwamba serikali wilayani humo inaendelea kufanya uchunguzi juu ya malalamiko
anayolalamikiwa Kaimu Ofisa ushirika wa wilaya hiyo, Kanisius Komba ambayo
yanatoka kwa wakulima wa vyama vya ushirika wilayani hapa na pale
itakapobainika kuna ukweli juu ya tuhuma anazonyoshewa kidole na wakulima hao hatua kali za
kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.
Cosmas Nshenye. |
Aidha Nshenye alifafanua kuwa wakulima wengi wamekuwa
wakimtuhumu kwamba amekuwa hatimizi majukumu yake ya kazi za ukaguzi wa vyama
hivyo ipasavyo, badala yake anadaiwa kushirikiana na viongozi wa vyama vya
ushirika kuhujumu vyama hivyo visiweze kusonga mbele kimaendeleo.
Kadhalika alidai kuwa wanaushirika hao wamekuwa wakimtuhumu
kwamba ni mtu ambaye anapenda kushiriki katika vitendo vya rushwa na kupotosha
ukweli wa ripoti za ukaguzi wa vyama hivyo.
“Hamna pasipo na ushirika Mbinga hii asipolalamikiwa, suala
hili lipo tunaendelea kulichunguza taarifa za ukaguzi amekuwa akizifanyia
ujanja ujanja na amekuwa sio mtu mkweli katika masuala ya ukaguzi analalamikiwa
na watu wengi”, alisema Nshenye.
Pia Nshenye alieleza kuwa chama cha ushirika kimojawapo wanachomlalamikia
wilayani humo ni Longa AMCOS ambapo wanachama wa ushirika huo katika msimu wa
kilimo mwaka 2015 walichukua mkopo wa shilingi milioni 50 kutoka benki ya NMB
lakini Wajumbe wa bodi ya ushirika huo kwa kushirikiana na Kaimu Ofisa ushirika
huyo, Komba wanadaiwa kushirikiana kwa pamoja kuhujumu fedha hizo.
Alisema kuwa fedha hizo zilikuwa zitumike kununua pembejeo za
kilimo kwa ajili ya wakulima katika msimu huo, lakini pembejeo zilizonunuliwa zilikuwa
ni za shilingi milioni 14,000,000 tu na fedha zilizobakia hazieleweki zimepelekwa
wapi na kufanya kazi gani.
Vilevile alisema kuwa ofisi yake ilipoona malalamiko hayo yamekuwa mengi kutoka katika vyama hivyo vya ushirika vilivyopo wilayani Mbinga, sasa wanafanya uchunguzi ili kuweza kupata ukweli wa malalamiko hayo na wahusika waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Vilevile alisema kuwa ofisi yake ilipoona malalamiko hayo yamekuwa mengi kutoka katika vyama hivyo vya ushirika vilivyopo wilayani Mbinga, sasa wanafanya uchunguzi ili kuweza kupata ukweli wa malalamiko hayo na wahusika waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
No comments:
Post a Comment