Na Kassian
Nyandindi,
Mbinga.
HALMASHAURI ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imechukua hatua
ya kumsimamisha kazi Kaimu Mhandisi wa idara ya ujenzi wilayani humo, Anyitike Kasongo kutokana
na kubainika kufanya makosa ya uzembe na ubadhirifu wa mali za umm
Anyitike Kasongo. |
Aidha imeelezwa kwamba kusimamishwa huko ambako ni kwa muda
usiojulikana kunalenga kupisha uchunguzi na baadaye atachukuliwa hatua za
kinidhamu kwa mujibu wa sheria na taratibu husika.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga, Gombo
Samandito alisema hayo alipokuwa akizungumza juzi na waandishi wa habari ofisini
kwake.
Samandito alisema kuwa sababu ya kusimamishwa huko anadaiwa
kufanya ubadhirifu na wizi wa mali za umma katika kazi ya ujenzi wa kibanda cha
mlinzi chenye thamani ya shilingi milioni 19,000,000 kwenye nyumba ya kuishi
Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Mbinga ambayo imejengwa mtaa wa Kipika mjini
hapa.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa Kaimu Mhandisi Kasongo
amesimamishwa kazi kwa sababu pia ya kufanya uzembe na kutotekeleza majukumu
yake ya kazi alizopewa ipasavyo, jambo ambalo limesababisha hata mwajiri wake
apate hasara kutokana na kibanda hicho kujengwa chini ya kiwango.
Vilevile ananyoshewa kidole kwamba alifanya mapokezi ya vifaa
ambavyo hakuvipeleka katika eneo la ujenzi wa kibanda hicho na kwamba jambo
hilo lilibainika baada ya kufanya ukaguzi wa ndani.
“Fedha hizi zilikuwa ni sehemu ya manunuzi ya vifaa vya
ujenzi wa kibanda hiki lakini muda mwingi alikuwa akionekana yeye akifika hapa
dukani kuja kuchukua vifaa vya ujenzi sasa tunashangaa kwa nini ameshindwa
kukamilisha ujenzi huu kwa viwango vinavyotakiwa wakati kuna vifaa vingi
alivichukua”, kilisema chanzo chetu.
Mhandisi Kasongo alipotafutwa na mwandishi wetu ili aweze
kutolea ufafanuzi juu ya jambo hilo hakuweza kupatikana na simu yake ilikuwa
ikiita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
No comments:
Post a Comment